Header Ads

Shabikia amchanganya Selena Gomez kisa Justin Bieber

SHABIKI mmoja ambaye jina lake halikufahamika, hivi karibuni alimchanganya staa wa R&B, Selena Gomez baada ya kung’ang’ania bango lililomtaka aolewe na mpenzi wake wa zamani, Justin Bieber. Katika bango hilo lililokuwa limeandikwa; 

Tafadhali olewa na Justin, lilimzuzua bi’dada huyo na kuamua kumuita shabiki huyo jukwaani kisha kuchukua bango hilo na kulitupa. Hata hivyo, kupitia ukurasa wa Twitter wa Selena, shabiki mwingine alitupia kipande cha video ya shoo hiyo na kumtaka Selena aolewe na Justin la sivyo atachukia na kulia. Selena na Bieber waliachana miaka miwili iliyopita huku chanzo kikitajwa kuwa ni usaliti katika penzi lao.

No comments