• Latest News

  May 11, 2016

  Snura: Chura imeniongezea umaarufu

  STAA wa Muziki wa Kizazi Kipya, Snura Mushi amefunguka kuwa licha ya changamoto ya kutakiwa kutengeneza video mpya yenye maadili ya wimbo wake wa Chura, umaarufu wake umeongezeka kwani jina lake limekuwa gumzo kila kona nje na ndani ya nchi. 
   
  Akipiga stori na gazeti hili, Snura alisema tangu aanze muziki hajawahi kufanya mahojiano na watu wengi kama kipindi hiki, kwani japokuwa alitakiwa na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kurekebisha wimbo huo, amepata faida kubwa kimuziki na kiakili.

  “Ukiachana na changamoto nimefarijika sana kwani jina langu limekuwa gumzo kila kona, nimepata elimu ambayo sikuwa nayo ambapo wizara imenipa ubalozi wa kuwafundisha wenzangu wasitoe nyimbo zisizokuwa na maadili, hivyo kila ninapokutana na wasanii wenzangu nawafundisha,” alisema
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Snura: Chura imeniongezea umaarufu Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top