Header Ads

Tiffah wa Diamond familia yadaiwa kushinikiza apimwe upya DNA Muhimbili!Hali inazidi kuwa hali! Yapo madai kwamba, familia, kwa maana ya ndugu, ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ wamemshauri msanii huyo kufanya kipimo tena cha vinasaba (DNA) kwa mtoto wake, Latiffah ‘Tiffah’ aliyezaa na Zarina Hassan ‘Zari’, Amani limenyetishiwa. 


Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndugu hao wamemtaka Diamond akubaliane na ushauri huo kwa kufanya kipimo hicho katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar ili majibu yake yawatie moyo ndugu ambao bado wanakubaliana na maneno ya mitandaoni kwamba, mtoto huyo si wa Diamond.
 

TWENDE NA CHANZO “Ndugu wengi wanajua Tiffah ni mtoto wa Diamond, lakini kuna wengine wanakubaliana na mitandao kwamba si wake.


 Sasa sisi ambao tuko sambamba na Diamond tunamshauri, ile DNA ya kwanza alipima Afrika  Kusini, majibu yakawa poa, apime nyingine Muhimbili. “Tunaamini kwa sababu ni Muhimbili ni nyumbani Bongo, majibu yakitoka hayatakuwa na kero wala maswali. 

Maana kule Sauzi wakasema ohoo! Zari alisimamia shoo kwa daktari wake wakiamini majibu yalipangwa,” kilisema chanzo hicho. Kiliendelea kwa kuhoji: “Lakini pia kwenye baadhi ya magazeti waliandika kwamba, DNA ya Tiffah, Afrika Kusini ni magumashi! Sasa kwa nini huu umagumashi unaosemekana kuwepo usitoke kwa kupima tena Muhimbili?”
 

NDUGU NUSU KWA NUSU “Hali ya mtoto Tiffah ina sitofahamu nyingi kwa baadhi ya wanandugu licha ya kwamba Diamond alishasema anachokiamini. Ndugu nusu
 wanaamini, nusu kama hawaamini. Lakini mtoto kusema kweli anaendelea vizuri sana,” kilisema chanzo hicho.
 

TIFFAH AANZA KUTEMBEA Habari zilizotua kwenye dawati la gazeti hili zinasema kuwa, tayari mtoto huyo ameanza kujifunza kutembea kwa kushikishwa vitu vyenye msaada kama vile baiskeli za watoto.
 

ZARI ATUMBUKIA NYONGO Habari zaidi zinasema kuwa, Zari alipoondoka jijini Dar hivi karibuni kuelekea Sauz hakuwa sawa na familia hiyo kwa mambo mbalimbali hususan kwenye ishu ya kukubalika na ndugu wa Diamond. “Zari aliondoka kwenda Sauz akiwa na Diamond, lakini kusema ule ukweli hakuwa sawa na familia. Kuna mengi ambayo hakuyapenda.

 Amejua familia ya mzazi mwenzie huyo ina dalili zote kwamba haimkubali. 

Hivyo Zari aliondoka kama mtu asiyetaka kurudi tena,” kilisema chanzo.
AMANI LAMSAKA MAMA DIAMOND Ili kupata mzani wa madai ya habari hii, gazeti hili lilimsaka mama wa Diamond, Sanura Kasimu
‘Sandra’ na kumsomea ‘mashitaka’ yote ambapo alisema: “Nyie nani kawaletea umbeya huo

Amani: “Vyanzo vyetu ndiyo chimbuko cha habari.” Mama Diamond: “Unaonaje kama utampigia simu huyohuyo aliyekuletea umbeya ndiyo uongee naye?” Akakata simu bila kusubiri majibu ya gazeti.
 

DIAMOND HUYU HAPA Diamond alipotafutwa juzi na kuulizwa kuhusu ishu hiyo alisema: “Kwani kama mtu haamini mimi nifanye nini? Ina maana kila kitu changu lazima nikiweke wazi?!” Amani: “Vipi kuhusu Zari kuondoka?” Diamond: “Ishu nini kwani? Yule mama wa mtoto wangu, unasikia!”
 

KUMBUKUMBU YA FIGISUFIGISU Agosti mwaka jana, Zari alijifungua Tiffah kwenye Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, lakini tangu mgeni huyo aje, kumekuwa na maneno kwamba, Diamond alibambikiwa. Madai yalijaziwa na mitazamo kuwa Zari alizaa mtoto huyo kwa mimba ya aliyekuwa mumewe, Ivan Ssemwanga, mfanyabiashara anayeishi Sauz. 

Mbaya zaidi katika kuchagiza madai hayo, inasemekana hata Ivan mwenyewe amekuwa akichangia kwenye mitandao ya kijamii kuhusu madai hayo. Kwa upande wake, Diamond amekuwa akipambana na utetezi kuwa, Tiffah ni bintiye kipenzi bila shaka wala kujazia maswali huku akisema wanaodai kabambikiwa wamekosa cha kufanya. Hata hivyo, miezi ya hivi karibuni, gazeti hili liliwahi kuandika habari yenye kichwa kisemacho; 

DIAMOND, TIFFAH WAPIMA DNA SAUZ! Katika habari hiyo, ilidaiwa kuwa, Diamond aliamua kupima kipimo hicho kama sehemu mojawapo ya utaratibu wa kawaida kwa nchi kama Sauz ambapo si mpaka mzazi awe anataka uhakika wa mtoto huyo kama ni damu yake au la!

CHANZO: GAZETI LA AMANI

No comments