Header Ads

Viashiria 11 kuwa mpenzi wako anakuhitaji faragha!

BILA shaka mpenzi msomaji umzima bukheri wa afya, huna budi kumshukuru Maulana kwa kukufikisha hapo ulipo na leo umeweza kukutana nami kwenye kujadili mada hii kuhusu viashiria 11 kuwa mpenzi wako wa kike anakuhitaji faragha.
Kiuhalisia wanawake wengi wameumbwa na hulka ya aibu, kiasi kwamba ni ngumu sana kusema moja kwa moja pale anapohitaji kukutana nawe faragha. Hivyo sehemu kubwa ya sema yao huwakilishwa na vitendo;
Macho
Macho ya mwanamke yanazungumza sana kwa kitu anachohitaji, ukijaribu kuyachunguza vizuri macho yake kuna kitu utakiona kinaashiria katika mboni za macho ya mpenzi wako, kama vile yanasinzia au yanakuwa kama amekula kitu kinachomfanya apatwe na kiusingizi cha mbali. Hii ni moja ya dalili.
Nimekumiss sana mpenzi wangu
Anaweza asiseme moja kwa moja lakini neno nimekumisi kwake likawa ni zaidi ya kumbukumbu kama ambavyo wengi wamelizoea, kumbe yeye akawa anamanisha amekumisi kwa maana ya kukuhitaji.
Mazungumzo
Ukijaribu kusikiliza sehemu kubwa ya mazungumzo yake ni kama huyaelewi vile, mara kasema hiki mara kile, hizo ni dalili kuwa anahitaji haki yake ila hawezi kusema.
Uchokozi wa hapa na pale
Wakati mwingine anaweza kuanzisha uchokozi ambao kimsingi anafahamu atakukera au kukukwaza pamoja na kumkataza bado akaendelea tu kufanya huku anacheka tena kicheko kama cha kejeli vile, shtuka weweee!
Hatulii
Kama mko ndani unaweza kumuona mwenzako hatulii, mara nyingi anakuwa anachezea viganja vyake kwa kuvisungua au kuchezea kucha zake.
Stori za kukufurahisha
Unaweza kushangaa mbona leo kachangamka sana au kafurahi kupita siku nyingine na pengine siku hiyo anapiga stori za kutosha na kufurahisha mpaka unamshangaa.
Kukusikiliza kwa upole
Unaweza ukaongea sana lakini muda wote akawa makini kukusikiliza kwa kila unachokizungumza kiasi cha kushangaa na tena anakuwa ni mpole kupindukia.
Maongezi yenye bashasha
Wakati mwingine hata maongezi yake yanakuwa yamejaa bashasha, hana haraka na wewe wala hata hakumbuki kama kuna kazi nyingine anapaswa kufanya.
Ukimgusa hachukii
Kama ikitokea ukapeleka mkono wako kwenye moja ya kiungo chake basi hatajisumbua kukutoa bali anaweza kujifanya kama vile hujamgusa.
Sitaki, nataka!
Mnaweza mkakubaliana kitu lakini ndani ya dakika mbili akageuka na kusema jambo lingine ila kukaa kwake anakuwa hajamaanisha bali ni mbwembwe tu za kike.
 Aina ya uvaaji
Nguo nazo zinaweza kumsemea mpenzi wako kile anachohitaji. Kwa mfano kaenda kuoga kisha kaja na nguo nyepesiii au anaweza kujifanya kakaa vibaya bila kukusudia,ukiona hivyo ujue kuna kitu anahitaji kwako!
Ni hayo tu kwa leo ni imani yangu kwamba utakuwa umepata elimu ya kukusaidia kumsoma mpenzi wako kupitia matendo yake anapokuhitaji.

No comments