• Latest News

  May 12, 2016

  Vodacom Tanzania yazindua mtandao wa 4G wenye kasi zaidi  Uzinduzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


  Akiongea kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema kuwa spidi ya mtandao wa 4G wa Vodacom haina tofauti na ile inayopatikana kwenye nchi zilizoendelea.
  Alisema kuwa mtandao huo utatumika kama chachu ya maendeleo kwenye sekta nyingi nchini.
  “4G kwetu sio teknolojia, 4G kwetu ni kiwezeshaji, ni kiwezeshaji kwa serikali, kiwezeshaji kwa biashara, ni kiwezeshaji kwa watumiaji wetu,” alisema. “Inachofanya inafungua fursa mpya, uwezekano mpya,” aliongeza.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Vodacom Tanzania yazindua mtandao wa 4G wenye kasi zaidi Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top