Header Ads

Wabunge vigogo waanguka NEC ya CCM

UCHAGUZI wa kuwasaka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kutoka kundi la wabunge, umefanyika huku baadhi ya vigogo wa chama hicho wakiambulia patupu.Uchaguzi huo ulifanyika juzi usiku katika ukumbi wa CCM mjini hapa, ambapo wajumbe waliwachagua Munde Tambwe alipata kura 163, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki (152) na Agnes Marwa, akipata kura 120.

Waliobwagwa ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Angelina Mabula aliyepata kura 84 na aliyekuwa Waziri wa Tamisemi katika Serikali ya awamu ya nne, Hawa Ghasia aliyepata kura 109.
 

Kwa upande wa wabunge wa Zanzibar, waliochaguliwa kuingia kwenye NEC ni Faida Mohamed Bakari na Jamal Kassim Ali.
 

Kwa upande wa kundi la wanaume waliochaguliwa ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, Mbunge wa Nzega Vijijini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya 

Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kingwangalla pamoja na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba.
Wengine ni Mbunge wa Maswa Mashariki, Stanlaus Nyongo na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani.
 

Waliobwangwa katika uchaguzi huo ni Mbaraka Kitwana Dau, Alex Raphael Gashaza, Ibrahim Hassanali Raza, Profesa Norman Sigalla King, Almas Maige, Angelina Malembeka.
Wengine ni Yahaya Massare, Mattar Ali Salum, Peter Serukamba na Hafidh Ali Tahir.
 

Kwa upande wa nafasi ya Katibu wa wabunge wa CCM aliyechaguliwa ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza, ambaye aliwashinda wapinzani wake Mary Chatanda, Mariam Kisangi na Abdallah Ulega.
CREDIT: NIPASHE

No comments