Header Ads

Wastara agoma kuolewa na kijana!

Mahari yaliyotolewa wiki mbili zilizopita kwa staa wa filamu Bongo, Wastara Juma, yamerudishwa kwa mwanaume aliyetaka kumposa, Juma Mbega, kwa kile kilichodaiwa kuwa msanii huyo amepinga vikali kuolewa na kijana huyo ambaye naye ni mwigizaji wa sinema za Kibongo. 
  1.  
Wiki mbili zilizopita Mbega alimtuma mshenga wake, Hamis Ramadhan kwenda kwa akina Wastara kupeleka mahari ya shilingi milioni tano, akitaka kumuoa staa huyo baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na Mbunge wa Donge kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sadifa Juma. Akizungumza kwa uchungu, Mbega alisema kuwa aliumia kupokea habari mbaya kutoka kwa mshenga wake huyo kwamba mwanamama huyo aliyarudisha mahari hayo na kwamba hataki kuolewa kwa sasa.

 “Namjua Wastara vilivyo, nilitamani sana mwanamke kama yeye kwa kuwa najua wengine hawawezi kuishi naye kwa upendo zaidi ya aliyekuwa mtu wangu wa karibu, marehemu Sajuki (Juma Kilowoko) na mimi mwenyewe,” alisema Mbega aliyekuwa rafiki mkubwa wa Sajuki. Mbega alisema kuwa, pamoja na kurudishiwa mahari, lakini bado hajakata tamaa ya kumfukuzia Wastara kwani anaamini ndiye mwanamke wa maisha yake. 

“Sijakata tamaa, naamini ipo siku atakubali, najua wazi hakuna mtu atakayemfaa zaidi yangu,” alisema jamaa huyo. Kwa upande wake Wastara, alisema aliyarudisha mahari kwa kuwa Juma ni kama mdogo wake aliyemlea hivyo asingeweza hata siku moja kukubali kuolewa naye. “Jamani yule nimeona ni kama mdogo wangu ndiyo maana nimerudisha mahari yake na siwezi kuolewa naye,” alisema Wastara. Kabla ya kuibuka kwa Mbega, Wastara alivurugana na Sadifa ambapo kila mmoja alichukua hamsini zake.
CREDIT; GPL

No comments