Header Ads

Wema, Gigy Money vita ya penzi la Idris....Gigy atamba kumchukua mchana kweupe!

 Juzikati lilifanyika bonge la pati pale Regency Hotel, Mikocheni jijini Dar lililokwenda kwa jina la Pool Party ambapo mbali na matukio mengine, msanii Gift Stanford ‘Gigy’ na mpenzi wa Wema Isaac Sepetu, Idris Sultan walisababisha gumzo baada ya kugandana kisha baadaye kudaiwa kuondoka pamoja. Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mashuhuda waliokuwa eneo hilo waliwaona wawili hao wakiwa ‘very close’ na hata wakati wa mapichapicha, mapozi yao yalikuwa tata huku Idris akishikilia ‘zigo’ la Gigy na mdada huyo naye kummiminia mabusu bwerere. 

 Msanii Gift Stanford ‘Gigy’akimbusu Idris Sultan.

ETI WAENDA KUMBONJI PAMOJA 
Washakunaku wakaendelea kushusha madai mazito kuwa, baada ya kutoka eneo hilo, Gigy alimganda Idris na kuondoka kwenda kumboji pamoja. “Walionekana kama mtu na mpenzi wake wakati tunajua Idris ni shemeji yetu kwa Wema. Hata kutoka, walitoka pamoja sasa utaona hapo kuna nini tena?” Alihoji mtoa habari huyo ambaye alidai ni shosti wa Gigy. 

HII NI VITA YA PENZI 
Kufuatia madai hayo, wachambuzi wa mambo walieleza kuwa, kitendo cha Gigy kujiweka kwa Idris huku akijua ni mpenzi wa Wema anataka kuibua vita ambayo inaweza kuleta madhara. Wakaeleza kuwa, ni siku chache tu Wema na Idris walikuwa na tofauti lakini wamezimaliza hivyo kama Gigy anataka bifu na Wema pamoja na timu yake, aendelee na uchokozi wake. “Hii ni kutaka kuleta ugomvi tu kwa kuwa, Team Wema hawawezi kukubali ‘Madam’ akaingiliwa, kama ametumwa na Team Zari ili kumtibulia mwenzake, kitakachompata asije akajuta,” alisema dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Zuu anayeonekana ni Team Wema ‘pure’. 
 

TEAM ZARI FULL KUSHANGILIA
 Ilibainika kwamba, baada ya Gigy kuonesha kutaka kumuingilia Wema kisha kupiga picha kibao za kiuchokozi akiwa na Idris na kuzitupia mtandaoni, kwa Team Zari imekuwa ni furaha na wamekuwa waki-tag picha hizo kwa kila anayejifanya ni Team Wema. Kufurahia kwa Team Zari kunakuja kufuatia hivi karibuni Team Wema kusherehekea baada ya kusikia kuwa, Zari aliingiliwa kwenye penzi lake baada ya binti aliyefahamika kwa jina la Irene ‘Lynn’ kudaiwa kutoka na Diamond Platnumz. 

MSIKIE GIGY 
Baada ya kunasa ubuyu huo, Ijumaa lilimsaka Gigy kwa udi na uvumba ili kuzungumzia madai ya kujiweka kwa Idris huku akijua ni shemeji yake kwa Wema ambapo alifunguka: “Mimi huwa siishi kwa kumuogopa mtu hata siku moja, ninachojua Wema hajaolewa na Idris hivyo sioni shida kuwa naye karibu na nikiamua hata mchana kweupe namchukua tu,” alisema Gigy. Alipoulizwa ni kipi ambacho anahisi Idris anaweza kuwa amevutiwa nacho kwake, Gigy alitiririka: “Mimi na Wema hatuna tofauti, kama ni mzigo (makalio makubwa) hata mimi ninao, kwa hiyo inawezekana Idris anapenda wanawake wenye makalio makubwa.” 

 MADAI YA IDRIS KUPENDA MIZIGO 
Hata kabla ya Idris kujiweka kwa Wema, iliwahi kudaiwa kuwa jamaa huyo anayepiga mzigo na Radio Choice FM anapenda sana wanawake wenye makalio makubwa na ndiyo maana hakuweza kudumu na ‘kile kidemu’ kutoka Sauzi (Afrika Kusini), Samantha Mumba. 

WEMA ANASEMAJE?
 Baada ya kusikia upande wa Gigy, waandishi wetu walimgeukia Wema ili azungumzie madai ya Gigy kummegea penzi lake lakini simu yake kila ilipopigwa haikuwa hewani. 
 
IDRIS HUYU HAPA 
Kufuatia madai hayo mazito ya kuchepuka, Ijumaa lilimtafuta Idris na alipopatikana mahojiano yalikuwa hivi: Ijumaa: Inakuwaje ‘Big Blaza’? Idris: Shwari tu, lete stori. Ijumaa: Stori ni kwamba, juzikati kwenye ile pati pale Regency Hotel ulimsaliti Wema kwa kuwa ‘vere klozi’ na yule mdada aliyefungashia yule. Idris: Nani huyo? Ijumaa: Gigy Money, na ikadaiwa licha ya kujiachia, eti mliondoka na kwenda kumbonji pamoja. Idris: Hahaaaa! Acha mambo yako bwana, mimi na Gigy wapi na wapi? Ijumaa: Ndiyo habari ya town na inasemekana umedatishwa na lile zigo lake. Idris: Hayo maneno ya watu bwana, mimi niko na Wema ila pale kwenye ile pati nilipiga naye picha si unajua mashauzi yake, ikaishia pale. Ijumaa: Kwa hiyo wewe na Wema sasa freshi na hakuna figisu? Idris: Yeah, tupo poa kabisa na hamna shida, hayo mengine ni maneno ya watu tu.

CREDI: IJUMAA GAZETI

No comments