Header Ads

Wema Sepetu afanyiziwa na Vijana wa kihuni kisha kuporwa simu na fedha

 Muigizaji mwenye wingi wa matukio Bongo, Wema Sepetu ‘Madame’ amekiri kufanyiziwa na vijana wa kihuni hivi karibuni, baada ya kutembezewa kichapo kisha kuporwa simu na fedha zilizokuwemo ndani ya gari lake, maeneo ya Mbezi Africana.


 Akizungumza  kwa njia ya simu, Wema alisema ni kweli tukio hilo lilitokea, baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongwa kwa nyuma na aliposhuka ili kuzungumza na mwenzake juu ya ajali hiyo, ndipo hali ya hewa ilipobadilika. “Usiku huo tulikuwa na Muna kwenye gari, mtu akaigonga kwa nyuma, tukashuka ili kuelewana lakini cha kushangaza tuliona vijana wakijazana ambao walipora pochi zetu zilizokuwa na fedha.

 “Kwenye pochi nilikuwa na simu na dola 2500 na Muna alikuwa na dola 3000ambazo zote ziliibwa na mpaka sasa hatujafanikiwa kupata chochote kati ya hivyo vitu,” alisema Wema.

 Awali, chanzo chetu kililiambia gazeti hili kuwa Wema alionekana kama aliyekuwa ‘ameburudika’ kwani mazungumzo ya maelewano na dereva mwanaume aliyemgonga yalikosa kufi kia muafaka na kumfanya Miss Tanzania huyo wa zamani, kupandisha munkari na kutoa maneno yasiyofaa, yaliyowasogeza vijana wa kihuni waliokuwepo eneo hilo. 

Kilisema vijana hao walichukizwa na maneno ya Wema na hivyo kuanza kumfanyia vitendo vya kidhalilishaji, kumpiga na baadaye kuingia ndani ya gari na kuondoka na vitu hivyo.

 “Yaani huku Afrikana na Salasala habari ya mjini ni Wema, kesho yake alikuja na difenda la polisi lakini hawakuambulia chochote,” kilisema chanzo hicho.

No comments