Header Ads

Wolper Ahofia Picha Zake za Utupu Kuvuja kutoka kwa mpenzi wake wa zamani!


Jacqueline Wolper akiwa na mpenzi wake .
Yamemkuta! Nyota wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper Massawe yuko katika wakati mgumu kufuatia kuahidiwa na mtu aliyetajwa kuwa ni mpenzi wake wa zamani akimtishia kuvujisha picha zake za utupu.
Kwa mujibu wa chanzo cha ‘Ubuyu Ulionyooka’, Wolper kwa sasa hana raha kwani zilipendwa wake huyo (hakutajwa) amekuwa akimwambia kuwa, kama hawatarudiana atavujisha kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii picha hizo alizowahi kumfotoa siku za nyuma.

AONEWA HURUMA
“Ninyi Wolper anatia huruma sana. Unajua nini, kuna mwanaume aliwahi kuwa mpenzi wake kwa siku kadhaa nyuma huko. Sasa nasikia siku moja, wakiwa wametoka klabu (jijini Dar), kufika chumbani, jamaa akachukua simu yake ya kiganjani na kumpiga picha Wolper,” kilidai chanzo hicho.
NI KWELI WOLPER ALIKUJA JUU?
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Wolper alimjia juu jamaa yake kuhusu kumpiga picha akiwa mtupu lakini jamaa akatumia lugha laini kwamba hajapiga kwa nia mbaya bali ni kumbukumbu.
“Jamaa yake alijitetea kwamba, picha hizo ni kumbukumbu tu hata siku akiwa nje ya nchi kwa safari zake atazitumia kuziangalia ili kumkumbuka, Wolper akalainika,” kilisema chanzo hicho.
Harmonize-3Harmonize
HOFU YA WOLPER IKO WAPI KWANI?
Habari zaidi zinasema kuwa, vitisho vyote hivyo, Wolper amepewa na bwana’ke huyo baada ya kubainika kuwa, amehamishia penzi kwa msanii wa Bongo Fleva, Rajabu Abdulhan ’Harmonize’ na kutoonesha dalili ya kurudi nyuma.
NI YULE MKONGO AU KUNA MWINGINE?
Wikienda lilimuuliza mnyetishaji huyo kama mwanaume mwenyewe aliyedaiwa kumpiga picha Wolper ni yule Mkongo?
“Mimi sijatajiwa jina. Kwa hiyo kama ni Mkongo au ni nani sijui, ila ni mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wake,” alisema.
WOLPER YEYE UNASEMAJE?
Ili kuweka sawa mzani wa ubuyu huo, juzi Wikienda lilimsaka Wolper na kumuuliza kuhusu uwepo wa wasiwasi huo na nini mtazamo wake kwa mtu huyo.
Wolper: Ni kweli kabisa. Hayo yote uliyoambiwa ni kweli. Jamaa niliwahi kuwa naye, amechukizwa sana na mimi kuwa na Harmonize. Kwa hiyo ametishia kwamba kama sitarudi kwake, atazivujisha picha hizo kwenye mitandao.
ILIKUWAJE?
“Siku moja tulitoka klabu. Unajua tena mambo ya mtoko, nilikuwa nimechangamka kiasi chake. Kufika nyumbani, kitandani mimi nikajitupa, nikajiachia, akanipiga picha.
“Ingawa nilikuwa na pombe zangu kichwani lakini niliweza kujua, nikamuuliza akasema eti amenipiga picha za kumbukumbu. Yakaisha.
“Sasa hivi karibuni ndiyo kaja na sera hizo za kuzivujisha kwenye mitandao ya kijamii ili kunichafua na kuniondolea heshima yangu kwa watu.”
NINI MTAZAMO WAKO?
“Mimi mtazamo wangu ni mmoja tu, nimekwenda kutoa taarifa polisi (hakutaka kutaja kituo) ili ikitokea wawe wanajua mapema.”
KWANI SI KUNA SHERIA YA MAKOSA YA KIMTANDAO?
“Ndiyo maana nikaenda polisi kwa sababu ya kuwepo kwa hiyo sheria. Siku ikitokea, polisi watajua waanzie wapi kumkamata.”
NI MKONGO?
“Mimi kwa leo (Jumamosi iliyopita) sitaki kumtaja jina lakini anajijua na anajua hataniweza katika hili, namuahidi akae akijua mapema.”
UHUSIANO WAKO NA MKONGO VIPI?   
“Sitaki hata kumsikia. Yeye ana maisha yake kwa sasa. Mimi nimejipanga kivyangu na yeye atakuwa kivyake. Maisha ndivyo yalivyo.”

CHANZO: GPL

No comments