Header Ads

Wolper: Mchumba wangu hataki nivae kiume


DIVA wa filamu za Tanzania, Jacqueline Wolper, amedai mchumba wake hataki kumuona amevaa mavazi ya kiume hivyo itamlazimu kuyavaa katika kazi tu na siyo kwenye mitoko.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Wolper, alisema toka akiwa mtoto mdogo alikuwa anavutiwa na mavazi ya kiume kwa sababu yanamtoa bomba kuliko mavazi ya kike.

“Nikilazimika kwenye filamu nitavaa tu kiume ila siyo kwenye mitoko yangu, napenda kuvaa ila mchumba wangu hapendi ndiyo maana siku hizi sionekani nikiwa nimevaa mavazi hayo,” alisema Jacqueline.

No comments