Header Ads

Yanga yafanya kufuru kwa Kessy

IMEBAINIKA kuwa Yimelazimika kuvunja benki ili kumnasa beki wa Simba,
Hassan Kessy, ambaywake ulikamilika juzi Jumamosi na kumpa mkataba wa miakmiwili akiwa amefanyiwa mambo ambayo unaweza kusema ni kufuru.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa beki huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, amesajiliwa kwa dau la Sh milioni 40.
 


Mbali na dau hilo, Yanga imempangia nyumba yenye hadhi nzuri na kumlipia kodi yote ya miaka miwili ili kumfanya aishi kwa uhakika sehemu iliyo na mazingira mazuri. Awali,
Kessy aliwahi kuwa na mgogoro na Simba hadi akagomea kucheza kutokana na kutompatia nyumba kama walivyokubaliana, jambo ambalo Yanga wamelitimiza bila wasiwasi.
 

Taarifa hizo zinasema kuwa mbali na kumfanyia yote hayo lakini Yanga imeingia makubaliano na mchezaji huyo kuwa itakuwa ikimlipa mshahara wa shilingi
milioni mbili kwa mwezi.
 

Alipotafutwa meneja wa Kessy Athuman Tippo ‘Zizzou’ ili kuthibitisha taarifa hizo hakuwa tayari na kusema kuwa ataziweka wazi mara tu mkataba wa Kessy na Simba utakapomalizika rasmi.

“Siwezi kusema lolote kuhusua taarifa hizo kwani kwa sasa bado
Kessy ana mkataba na Simba, kila kitu kitakuwa wazi pale mkataba wake
utakapomalizika rasmi,” alisema Tippo.
Yanga ambayo ipo imara na inaelekea kutwaa ubingwa wa Ligi  Kuu Bara, inazidi kujiimarisha ili kufanya vizuri zaidi msimu ujao.


CHANZO; CHAMPIONI

No comments