Header Ads

Aunt Lulu auza mishikaki, bwana’ke amvunjia banda

 
Baada ya kutosikika kwa muda mrefu, Mtangazaji Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amevunja ukimya kuwa kilichosababisha awe kimya ni baada ya kufungua kibanda cha kuuza mishikaki ambapo alikuwa akiuza hadi nyama kilo tano kwa siku lakini amerudi nyuma kufuatia ugomvi na bwana’ke aliyemvunjia kibanda hicho kilichokuwa maeneo ya Kinondoni-Mahakamani, Dar.

 Sosi wa karibu na staa huyo, aliliambia Wikienda kuwa kuna kipindi Aunt Lulu alikuwa na maisha magumu hadi akaamua kuanzisha kibanda chake cha kuuza mishikaki kila siku jioni lakini banda lake lilivunjwa na bwana’ke huyo aliyekuwa akimpiga na kumzuia kufanya biashara hiyo. Kufuatia ishu hiyo, mwanahabari wetu alimtafuta Aunt Lulu ambaye alifunguka kuwa ni kweli alikuwa amefungua kibanda hicho cha kuuza mishikaki kwa sababu yeye ni mchakarikaji na alifurahi kwa muda kwa sababu alikuwa akiingiza fedha nzuri lakini kwa sasa amerudi kwa mama yake, Salasala jijini Dar baada ya kubomolewa kibanda hicho na mpenzi wake. “Sitaki tena wanaume, nilikuwa nimeanza kuchangamka kwani biashara yangu ilikuwa inanilipa lakini sijui bwana huyo aliona nafaidi sana, nimetulia kwa mama yangu, nitafungua biashara nyingine hukuhuku (Salasala),” alisema Aunt Lulu

No comments