Header Ads

Baba’ke Mdogo Kaka - 07

ILIPOISHIA : “Basi mwisho leo kusema umechoka halafu unachukua chumba hotelini, kwanza unamaliza pesa bure.”  Kule chini, Liana alikohoa mara moja kwa vumbi, mama yake akashtuka...  SHUKA NAYO SASA...
LAKINI Chidi aliunganisha haraka sana na kujifanya yeye ndiye aliyekohoa na akaendelea kukohoa huku akisema... “Yaani hali ya hewa hii, toka jana nakohoakohoa sana...” “Mi mwenyewe nakohoa...halafu nilifikiria kuna mtu anakohoa humu ndani, kumbe wewe.” “Mimi bwana.” Kule chini, Liana aliachia tabasamu mwenyewe kwani alipojikuta amekohoa, alijua ameumbuka na hakufikiria kama Chidi angeweza kuunganisha kwa staili ile na kuua soo! “Da! Namkubali baby wangu, yaani hapa nilishabainika kama siyo akili zake,” alisema moyoni Liana. Chidi alivaa ili waondoke... “Mbona sasa unavaa, una maana gani?” aliuliza mama Liana... “Si tunaondoka, au?” “Yaani mimi nimeingia mpaka chumbani halafu unataka tuondoke, hakuna kitu kama hicho,” alisema mama Liana na kumshika mkono
Chidi, akamrudisha kitandani na kumvua nguo, akampandisha kitandani... “Yaani unataka nitoke na tamaa yangu wakati wewe upo?” alihoji mwanamke huyo huku sasa na yeye akijichojoa nguo zake. *** Hali ya Liana ilibadilika, alianza kuhisi anaangalia picha ya x kwani mama yake wakati anapanda kitandani kuungana na Chidi, alibadilika sauti, ikawa ya kimahaba zaidi huku akisema maneno ambayo, yalimpa muwashawasha yeye. “Da! Mama naye...yaani kumbe yumo...da!” alijisemea moyoni Liana. Hali hiyo ilimpa wakati mgumu sana Liana kwani alikuwa kama yeye ndiye yupo kitandani na Chidi. Alivuta picha namna alivyoanza mchezo na Chidi na akatibuliwa na hodi ya mama yake. *** Mama Liana kazi yake kubwa ilikuwa kulalamika tu huku akimmwagia sifa kibao Chidi kwa kila hatua aliyokuwa akiifanya pale kitandani. Ilifika mahali alizidisha kulalamika mpaka Chidi akamshauri kupunguza malalamiko hayo. Lakini pia, Chidi alijua malalamiko ya mama huyo yanampa wakati mgumu, Liana kule chini. Ilifika mahali, mbwembwe za Chidi kwa mama yake zilimkera Liana kule chini kwani aliona kama anamfanyia kusudi wakati kumbe mwenzake alikuwa hali tete..! “Chidi ameamua kunikomesha, atakoma na mimi nitamkomesha mpaka aseme basi,” alisema moyoni
Liana. Mama Liana alipokuwa amekolea kwenye mchezo, alipiga kelele, Liana akajikunja kama amemwagiwa maji  ya baridi kwani alijua akiendelea kushirikiana na tukio hilo angeweza kutibua mambo. Na katika mambo ambayo alikuwa hataki mama yake ajue, ni kuhusu uhusiano wake na Chidi. Alijua mama yake akifahamu hilo, kwanza atamfukuza nyumbani, pili atamwachia laana, tatu atateseka na maisha ya mbeleni, nne ndugu wote watamtenga kwani hata kama Chidi ni mdogo kiumri tofauti na mama yake, lakini ndiyo hivyo, mama kapenda sasa..! Mchezo ulimalizika, mama Liana na Chidi wote walikwenda kuoga. Wakati wanaingia bafuni, Chidi alibaini kuwa, Liana alilala jirani sana na sehemu aliyoingilia kiasi kwamba, kama mama yake atatoka bafuni, ataweza kumwona japo kwa upande, hivyo alifunga mlango wa bafuni, akarudi, akainama... “Oyaa! Ingia ndani kabisa ukutani kule,” alimwambia Liana... “Poa, lakini ulichonifanyia Chidi siyo kizuri hata kidogo.” Chidi hakumjibu, akajua wataongea baadaye lakini akawa anawaza ni kitu gani alichokilalamikia Liana, hakupata jibu. Kule chini, Liana aliposikia mlio wa maji, akajua wameshaanza kuoga, huwezi amini alijipa ujasiri wa ajabu, akatoka haraka sana, akavaa haraka sana, akafungua mlango na kutoka huku akiurudisha mlango mpaka ulipobana. Alitembea kwa mwendo wa haraka mpaka mapokezi ambapo mhudumu alipomwona namna
alivyochafuka kwa vumbi, alishtuka kwani alijua alikuwa na Chidi na kuna shangazi mtu aliomba kuonana na Chidi... “Kwenda huko anti?” alimuuliza. “Kwema wapi! We unamwingizaje mtu kwenye chumba bila mawasiliano bwana!” alisema Liana akitoka nje kwa kasi. Baadhi ya watu walipomwona walimshangaa sana kwa namna alivyoonekana msichana mzuri lakini amechafuka kwa vumbi. Hata alipoingia kwenye gari, muuza duka alitamani kujua nini kilimpata lakini alikosa nafasi kwani, Liana aliliondoka gari kwa kasi. *** Baada ya kumaliza kuoga, mama Liana na Chidi walivaa, wakatoka lakini mama Liana alishtuka kugundua kuwa, mlango haukuwa umefungwa... “Baby, kumbe hatukufunga mlango! Yaani kama mtu angekosea chumba chake akaja kuingia kwetu ingekuaje? Si angejionea sinema ya bure!” mama Liana alimwambia Chidi huku yeye ndiye akifunga mlango ili funguo akaziache mapokezi... “He! Kweli? Loo! Leo tungeumbuka mke wangu,” alishangaa Chidi lakini hakujua kama Liana alitoka na hapo alikuwa akipiga akili ni vipi Liana atatoka. Walishuka wote mpaka chini, mapokezi huku mama Liana akiwa amemshika mkono Chidi kwa lengo la kumrusha roho, mhudumu, naye alipowaona, alishtuka, akamuuliza Chidi... Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma siku ya Jumatano. 

MTUNZI: IRENE M. NDAUKA

No comments