Header Ads

Bao la TP Mazembe offsideYANGA imeshindwa kutimiza ndoto yake ya kuwamaliza vigogo wa Afrika TP Mazembe katika michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0, jana. Katika mechi hiyo ambayo mashabiki waliingia bure kwenye Uwanja wa Taifa, Dar Yanga ililala kwa bao hilo la dakika ya 75, mfungaji akiwa ni Merveille Bope, lakini mchambuzi maarufu nchini Bakari Malima, amesema ni tata na linaonyesha ni offside (la kuotea). Malima aliyekuwa beki nyota wa Yanga, Simba na Taifa Stars, amesema kuna utata wakati Bope akifunga bao hilo kwa kuwa alikuwa mbele ya wachezaji wote wa Yanga lakini pia akawalaumu walinzi wa timu wa Yanga.
“Ukiangalia kuna utata, naona ni offside kwa kuwa mfungaji alikuwa mbele.

Unaona kabisa anamalizia wakati akiwa peke yake kabisa na mbele. “Lakini pia walinzi wa Yanga hawakuwa makini kwenye kukaba, walikaa mbali. Wakati mwingine ni vizuri kukaba tu na kuondoa utata wowote utakaotokea,” alisema Malima ambaye ni maarufu kama Jembe Ulaya.  Picha za video ambazo ‘zilikamatwa’ na kuwa mnato zinaonyesha Bope akifunga mbele ya mabeki wote wa Yanga. Pamoja na kwamba kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko alichelewa Kichuya apiga tizi saa 4 kwa ajili ya Simba Khadija Mngwai, Dar es Salaam

KIUNGO mshambuliaji wa Mtibwa Sugar anayetarajia kutua Simba, Shiza Kichuya yupo katika mazoezi makali ya saa nne kila siku ili kujiimarisha kuhakikisha anatoa ushindani wa kutosha msimu ujao. Kichuya ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa mbioni kusajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh milioni 20, ili kuisaidia timu hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kichuya amefunguka kuwa, tangu atoke Taifa Stars amekuwa mtu wa kupiga tizi kwa saa nne kwa siku katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Morogoro, mkoani Morogoro ili kuleta ushindani katika timu yake mpya.

“Nimeanza kufanya mazoezi binafsi kwa saa nne kwa siku tangu nilivyotoka katika kikosi cha timu ya
taifa lengo likiwa ni kujiimarisha na kuhakikisha naleta ushindani msimu ujao kama ilivyokuwa msimu uliopita nikiwa Mtibwa. “Haijalishi kama nitakuwa Simba ama nitabaki hapahapa (Mtibwa) lengo langu ni kuendelea kuwa fiti zaidi na kuleta ushindani na hata nikiwa Simba ninachohitaji ni kupata namba na sehemu yenye ushindani ndiyo ninayoipenda zaidi kwani inanisaidia katika kujiweka fiti,” alisema Kichuya.

kuondoka kwenye ukuta, lakini Bope bado anaonekana yu mbele yake wakati akimalizia kupiga mpira. Mabeki wa Yanga, Vincent Bossou, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Kamusoko mwenyewe, mshambuliaji Donald Ngoma pamoja na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ wanaonekana wakiinua mikono juu wakipinga kwamba mfungaji alikuwa ameotea. Lakini picha hizo pia zinaonyesha kuna tatizo la ukabaji kama ambavyo Malima amesema, kwamba mfungaji alibaki peke yake na baada ya piganikupige, akamalizia kwa urahisi kabisa akiwa karibu na Dida. Hata hivyo, Yanga iliweza kuonyesha soka la kuvutia na kuwapa TP Mazembe wakati mgumu huku Mtanzania, Thomas Ulimwengu akionekana kuwa mwiba kwa mabeki wa Yanga.

Yondani ndiye aliyemwangusha Ulimwengu nje kidogo ya boksi. Baada ya hapo faulo ilipopigwa, Yanga walionekana kama kuzubaa ingawa bado Bope kuwa mbele ya mabeki hao ndiyo kunazua utata huo. Yanga ilipoteza nafasi kadhaa kama ilipokuwa kwa TP Mazembe ambao walionyesha uwezo mkubwa hasa katika safu ya ulinzi ambayo iliwadhibiti vizuri washambulizi wa Yanga kama Ngoma, Obrey Chirwa na Juma Mahadhi ambaye alionyesha kiwango cha juu. Huu ni mchezo wa pili wa hatua ya makundi Yanga inapoteza kwa idadi hiyo baada ya kufungwa ugenini katika mechi ya kwanza dhidi ya MO Bejaia ya Algeria na sasa inakwenda mkiani. Akizungumza baada ya mchezo huo, Ulimwengu alisema: “Yanga walijitahidi, lakini sisi tulipata nafasi na tukaitumia vizuri.”

No comments