Header Ads

Barakah Da Prince: Nimsaliti Naj kwa Linah, sijipendi?

Barakah da Prince na mpenzi wake, Naj.


Juzikati wasanii Baraka Andrew ‘Barakah da Prince’ na Estelina Sanga ‘‘Linah’ walinaswa wakiwa kimahaba, tukio lililoibua gumzo na wengi kudhani mkali huyo wa ngoma ya Siwezi kachepukia kwa ndege mnana.
baraka na linah (2) 
Barakah da Prince na Linah.
Baraka na Linah walinaswa katika viunga vya Escape One kulikokuwa na shoo ya Christian Bella ambapo jamaa alionekana akimshikashika mdada huyo bila aibu.

Akilifungukia tukio hilo, Baraka alisema kuwa, yalikuwa ni mapozi ya kawaida tu na wala watu wasihisi anachepuka na Linah.

“Hivi nimsaliti Naj (Najma mpenzi wake wa sasa) sijipendi? Yale ni mapozi ya kawaida tu. Narudia tena, nampenda sana Naj na hakuna mbadala wake,” alisema Baraka.
 Stori: GABRIEL NG’OSHA

No comments