Header Ads

BINTI WA ALI AELEZEA MOYO WA BABA YAKE ULIVYOENDELEA KUFANYA KAZI KWA DAKIKA 30 BAADA YA VIUNGO VYOTE KUSIMAMA


Binti wa bondia gwiji, Muhammad Ali aliyefariki dunia leo, ameelezea namna moyo wa baba yake kuendelea kupiga kwa dakika 30 hata baada ya kila kiungo chake kuonekana kimetulia.

Hana Ali, amesema moyo wa baba yake uliendelea kupiga kwa dakika 30 baada ya kila kiungo chake kuacha kufanya kazi.

Binti huyo amesema waliendelea kumkumbatia na kumuombea Kiislamu huku mwisho akisisitiza wana furaha kwa kuwa baba yao amepumzika.

Ali ndiye bondia maarufu kuliko wote waliowahi kutokea katika historia ya ngumi za kulipwa duniani.
No comments