Header Ads

Brandy: Nimemnyima penzi kigogo, anatishia kuniua


MSANII wa Filamu Bongo, Brenda Godwin ‘Brandy’ ametoa la moyoni kuwa kuna kigogo wa serikalini amemuomba penzi na alipomkatalia amekuwa akitishia kumuua.
Akisimulia ishu nzima ilivyo, Brandy alisema kuwa: “Siku moja nilipigiwa simu na mwanaume ambaye alisema ni mdau wa filamu na alikuwa akitaka kufanya kazi na mimi.
“Kweli nilikwenda kuonana naye maeneo ya Posta ni mbaba anayeonekana anazo, akadai yupo serikalini.
“Kuanzia siku hiyo akawa ananisumbua, mara tukutane hotelini… nikajua huyu siyo, nikampotozea. Juzi kanitumia meseji ndefu akinitishia maisha, ndo’ najipanga kwenda kuripoti polisi.”

No comments