Header Ads

JEURI YA FEDHA, MASHABIKI WATAINGIA BURE YANGA VS TP MAZEMBE


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeamua mashabiki watakaoingia uwanjani kushuhudia mechi kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe, kesho Jumanne hawatalipa viingilio.

Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Yanga, sasa ni bure. Ikiwa hilo litatekelezeka, Yanga inaweza kupoteza zaidi ya shilingi milioni 300 ambazo zingeweza kupatikana kutokana na kiingilio cha mchezo huo.

manjiMwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji.

Awali, Championi Jumatatu lilipata taarifa hizo saa tatu usiku, jana lakini ilikuwa vigumu kuzithibitisha baada ya kuelezwa viongozi wa Yanga walikuwa kwenye mkutano akiwemo mwenyekiti wao, Yusuf Manji. Baadaye chanzo cha uhakika kikasema:“Kweli, wameamua iwe hivyo, mashabiki wataingia bure kabisa na wameombwa waende kwa wingi kuishangilia Yanga.” Juhudi za kuupata uongozi wa Yanga zilifanikiwa saa nne na nusu usiku na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji alithibitisha kwa mdomo wake. Championi: Kweli mmeamua mashabiki waingie bure?


Manji: Kweli viongozi tumekubaliana kwa umoja baada ya kukaa. Tunataka mashabiki wa Yanga na mashabiki wengine wanaopenda mpira bila kujali ni wa timu gani
wakashuhudie mpira.

Championi: Hamuoni Yanga itaingia gharama kubwa na kukosa kitu? Manji: Yanga ipo kwa ajili ya wananchi, Yanga ni furaha ya watu wengi.

yanga

Championi: Kuingia kwa mashabiki bure, wanaweza wakaingia wengi ambao ni adui wa Yanga, huoni itawaumiza?

Manji: Mashabiki wa Yanga ni wengi sana Tanzania. Bado hatuamini Wacongo wanaweza kuwazidi Watanzania kwa wingi. Hata watu wa Simba ni mashabiki kutoka Tanzania, waende wakaiunge mkono Yanga. Siku moja Yanga
watawaunga mkono wao wakiwa wanashiriki michuano ya kimataifa. Championi: Vipi kuhusu sehemu kama zile za VIP na nyinginezo?

Manji: Sijakuelewa, ila kama una maanisha kukaa. Kwa kuwa ni bure, watu wanaweza kuwahi na kukaa VIP, hakuna shida.

Championi: Kipi hasa kilichosa-babisha uamuzi huu? Manji: Tunahitaji mchezaji wa 12, lakini elewa huu ni uamuzi wa uongozi wa Yanga, pia ujue Yanga ni timu ya wananchi
na mafanikio yake ni furaha ya wengi. Ahsante.

Baada ya hapo, Manji hakutaka kuzungumza zaidi na kusisitiza kama kutakuwa na maswali zaidi, litakuwa ni suala la msemaji wa klabu, Jerry Muro. Pamoja na hivyo, taarifa zinaeleza uongozi wa Yanga umeandika barua kutaka Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuruhusu urushaji wa matangazo hayo kuwa nje ya Tanzania.

"Kweli inatakiwa hivyo, kwamba Caf wana haki lakini warushe nje ya Tanzania. Hapa watuachie sisi na kama hivyo unaona mashabiki wanaingia bure," alisema Muro kwa ufupi wakati tunaenda mitandaoni.

MurO MgENI rASMI Aidha, taarifa ambazo zilifika katika gazeti hili muda mfupi kabla ya kwenda mtamboni ni kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo anatarajiwa kuwa msemaji wao, Jerry Muro. Mtu wa karibu kutoka ndani ya uongozi wa Yanga alilithibitishia gazeti hili kuwa uamuzi wa klabu hiyo kumpa nafasi Muro umetokana na uwajibikaji wake klabuni pao. “Jerry ni mpambanaji na amekuwa akiipigania klabu kwa nguvu zake zote, hivyo kuonyesha tunathamini kazi yake na ndiyo maana viongozi wameamua awe mgeni rasmi wa mchezo huo wa Jumanne, ambapo yeye ndiye atakayekagua timu na majukumu yote ambayo mgeni rasmi anatakiwa kuyafanya,” alisema mtoa taarifa huyo.

No comments