Header Ads

Chuchu Hans adaiwa kunasa ujauzitoChuchu Hans.
STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans anadaiwa kunasa ujauzito wa mchumba wake ambaye naye ni staa wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’. Kwa mujibu wa chanzo ambacho kipo karibu na wawili hao, Chuchu kwa sasa ni mtu wa kujifungia ndani na amekuwa hapatikani kwenye matukio mbalimbali yanayomhusu. “Ameshanasa, tena ujauzito huo ni wa Ray, unaambiwa sasa hivi kawa mtu wa kujifungia ndani tu na kitumbo kimeshamtoka,” kilisema chanzo.
CHUCHU789111 
Chuchu na Ray
Alipotafutwa Chuchu kujua ukweli alijibu; “Nashangaa, watu wengi wananifikiria hivyo lakini sitaki kuongea chochote. Labda watakuwa na husda tu ndiyo maana wananifikiria hivi,” alisema Chuchu. Ray alipotafutwa kwa njia ya simu ili kusikia kauli yake hakupokea

No comments