Header Ads

ENGLAND WANG'OLEWA EURO NA ICELAND WACHAPWA BAO 2-1


Pamoja na kutokuwa na mafanikio makubwa sana katika michuano ya kimataifa, England ndiyo wanaongoza kwa kuwa na makelele mengi na jana, wameng’olewa kwenye michuano ya Euro kwa kuchapwa mabao 2-1.

Mabao hayo 2-1 yametoka kwa Iceland ambayo awali ilionekana ni kibonde na isiyo na uwezo.

Lakini imefanikiwa kuonyesha soka safi, ikitoka nyuma na kusawazisha halafu ikafunga bao la pili. England walianza mapemaa kwa bao la penalti la nahodha Wayne Rooney.


Lakini mwisho, England wakatoka na kuacha gumzo kwani Iceland inakwenda nusu fainali ikiwa iliingia katika michuano hiyo haipewi hata nafasi ya kuvuka hatua ya makundi.

No comments