Header Ads

G Nako Agoma Kuanika Uhusiano Wake

G Nako.
MKALI kwenye gemu la Muziki wa Hip Hop, Bongo, G Nako Wara Wara amegoma kuanika juu ya uhusiano wake wa kimapenzi  na kudai kuwa  suala hilo ni binafsi na hadhani kuwa kuanika mpenzi kutamsaidia lolote lile katika muziki wake.
Akipiga stori na mtandao huu G Nako aliongeza kuwa mara kwa mara baadhi ya mashabiki zake na wanahabari wamekuwa wakimuuliza juu ya hilo  lakini amekuwa  mgumu kufunguka na  ukifika  wakati ambao atadhani ni sahihi  kuweka wazi basi atafanya hivyo.
G Nako (1)
“Niko katika uhusiano wenye furaha,  hilo ndilo pekee watu wanatakiwa kufahamu,  lakini niko na nani, anajishughulisha na ishu gani si suala la msingi na wala haliniongezei lolote kwenye  kazi yangu,” alisema G Nako.

No comments