Header Ads

Gardner anaswa na mpenzi mpya wakiwa wamegandana jijini Dar

Miezi michache baada ya wanandoa Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na Gardner Gabriel Fikirini Habash kutalikiana kwenye Mahakama ya Mwanzo Manzese Sinza jijini Dar, mwanaume huyo amemuanika ‘mtu wake’ wa sasa a.ka. ‘mwendokasi’ akisema ndiye mrithi wa mikoba ya mwimbaji huyo nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya, Amani linakuunganisha na Gardner


BOFYA HAPA USIKIE MAMBO 
Katika Viwanja vya Escape One, Kawe, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, ambako mwimbaji mahiri wa Muziki wa Dansi Bongo, Christian Bella alikuwa akifanya shoo ya kutimiza miaka 10 katika ‘game’, Gardner alionekana na mrembo huyo akizunguka naye kimahaba kutoka eneo moja kwenda lingine huku wadau wake wakihoji ni nani! Wakati f’lani, Amani lililokuwepo katika shoo hiyo, lilimuona Gardner ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la Kapteni, akienda na mrembo huyo hadi sehemu alikokuwa amesimama Video Queen, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ambaye siku chache zilizopita ilidokezwa kwamba alikuwa akitoka kimahaba na mtangazaji huyo.
 

GARDNER ALICHOFUATA KWA GIGY
 Amani liliwasogelea watatu hao wakiwa wamesimama na maongezi yao kuonesha kuwa ni nyeti lakini lilifanikiwa kuwasikia. Ilikuwa hivi: Gardner: “Oya!
We Gigy, huyu ndiyo mtu wangu sasa. Puuza zile habari kwamba mimi na wewe ni wapenzi. Puuza kabisa.” Gigy: “Aaah! Sawa, mzima mwaya wewe?” Mwendokasi: “Mi mzima mwaya, wewe je?” Gigy: “Hata mimi mzima.” Baada ya maongezi yao ya utambulisho, Gardner aliondoka eneo hilo akiwa amemshika kiunoni msichana huyo.
 

CHA AJABU SASA
 Ili kujitosheleza, nje ya viwanja hivyo, siku iliyofuata, Amani lilimtafuta Gigy Money kwa njia ya simu na kumuuliza alijisikiaje kwa utambulisho ule. “Nakumbuka tulikuwa wote ndiyo pale Escape One, sisi huwa tunatoka pamoja, yule msichana namfahamu na amemfahamu Gardner kupitia mimi, wale ni washkaji wa kawaida tu, mimi ndiye mshkaji wa Gardner,” alisema mdada huyo katika jibu la kushangaza. Gigy ambaye jina lake linaanza kuwa kubwa licha ya kutofanya sanaa kwa kiwango hicho, aliongeza kuwa, asingeweza kuwazungumzia zaidi wawili hao, kwa vile kwake yeye haoni chochote cha muhimu zaidi ya kuwa ni marafiki wa kawaida.
 

HUYU HAPA GARDNER SASA 
Amani liliamua kumtafuta mtangazaji huyo ambaye wakati mwingine huwa ni ‘msema chochote’ kwenye shughuli (MC) na kumuuliza kuhusu ‘ubuyu’ huo wa Escape One. “Unajua nini kaka, siku ile kweli nilikuwepo, lakini unaponiambia una picha yangu nikiwa na msichana, siwezi kujua unaizungumzia picha gani, labda unitumie ili niweze kukujibu kitu cha
uhakika,” alisema Gardner. Bila kupoteza muda, alitumiwa mojawapo ya picha nyingi zilizopigwa akiwa na mdada huyo, lakini hakuleta mrejesho katika muda uliotarajiwa, ingawa alifanya hivyo dakika 45 baadaye. “Yes! Ndiye huyo kaka. Huyo ndiye mtu wangu kwa sasa na kama nilivyowahi kukudokeza, nimekuwa naye kwa muda mrefu kidogo, lakini sikuweza kumwanika mapema kwa sababu zinazoeleweka au ninazozijua mwenyewe,” alisema mtangazaji huyo maarufu ambaye ameshafanya kazi katika vituo vitatu vya redio, Clouds FM, Times FM na EFM. Amani: “Vipi kuhusu Jide sasa, ndiyo n’tolee moja kwa moja kwa sababu ya talaka?” Gardner: “Jide kitu gani bwana? Huyo ndo’ mwendokasi wangu kwa sasa.” Gardner alimtaja binti huyo aliyekataa kusema umri wake kuwa anaitwa Vestina Jax, mkazi wa jijini Dar es Salaam.
 

VIPI KUHUSU NDOA? 
Amani lilitaka kufahamu kama kuna mipango yoyote ya kufunga ndoa katika siku za karibuni baina yake na mrembo huyo, lakini Gardner alikataa kusema lolote juu ya hilo. “Duu! Acha basi kaka! Kwa hilo sina comment,” alisema mtangazaji huyo ingawa habari za ndani zaidi zinasema kuwa, mrembo huyo ndiye mkewe mratajiwa.   
CHANZO: GAZETI LA AMANI

No comments