• Latest News

  June 06, 2016

  GIGY ADAIWA KUVUNJA UCHUMBA WA MAN FONGO


   Msanii ambaye ni muuza nyago maarufu kwenye nyimbo za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’, anadaiwa kuvunja uchumba wa msanii anayetamba kwenye Miondoko ya Singeli, Amani Fongo ‘Man Fongo’ na mwandani wake Mariam Mfaume baada ya picha zinazowaonesha wakiwa kimahaba kuzagaa mtandaoni wakilinadi penzi lao.
   
  Kwa mujibu wa chanzo, siku chache zilizopita iliripotiwa kwenye gazeti ndugu la hili, Amani kuwa wawili hao wanatarajia kufunga pingu za maisha kabla ya Mfungo wa Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani, lakini ndoa hiyo imeyeyuka. Baada ya kuupata ubuyu huo, Wikienda lilimtafuta Mariam ambaye alisema chanzo cha yote ni picha kwani anaamini Gigy ‘anabanjuka’ na mumewe mtarajiwa hivyo hayupo tayari kuolewa na Man Fongo. Alipotafutwa Man Fongo, hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo kwa madai kuwa ni ishu ya kifamilia lakini kwa upande wake Gigy anayedaiwa kuwa na msururu wa wanaume mastaa alijibu kwa kifupi: “Kama wamemaindiana mimi hainihusu.”
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: GIGY ADAIWA KUVUNJA UCHUMBA WA MAN FONGO Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top