Header Ads

GIGY ANASA MWARABU, APIGWA STOP KUKAA NUSU UTUPU! MWEZI MTUKUFUVideo Queen wa Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ inadaiwa kamnasa mwanaume wa Kiarabu anayeishi Dubai aliyetajwa kwa jina moja la Aziz ambaye amempiga ‘stop’ kukaa nusu utupu hasa katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni moja ya mtihani aliyompa ambao endapo ataushinda atamuoa. Ubuyu kutoka kwa chanzo makini kilicho karibu na Gigy, kimeeleza kuwa mrembo huyo kwa sasa anapata wakati mgumu kuhakikisha hakosei kimavazi ingawa amekuwa akijisahau na kuvaa suruali za kubana ‘soksi’. 

“Hivi mnajua kuwa Gigy amepata bwana wa Kiarabu? Nasikia jamaa amempa masharti magumu kuhakikisha anavaa mavazi ya stara ndiyo amuoe. “Pia amemwambia kwa mwezi huu wa mfungo akiweza kujistiri, atapata nafasi kubwa ya kuwashawishi wakwe zake kwani amekuwa akipiga picha na kumtumia bwana
huyo anayeishi Dubai,” kilinyetisha chanzo hicho kwa ombi la kutoanikwa gazetini. Chanzo kilizidi kumwaga ubuyu kwamba, mwanzoni Gigy alikuwa akimdanganya jamaa huyo kwa kumtumia picha kisha anatumiwa fedha lakini bwana huyo ameonekana kuvutika na kumuomba ikibidi uhusiano wao uende mbele zaidi. “Kama mtamchunguza Gigy mtagundua siku hizi anajistiri tofauti na zamani ambapo kukaa utupu kwake ilikuwa kama fasheni,” kiliongeza chanzo hicho. Kama kawa, Wikienda liliponasa ishu hiyo lilimfuata Gigy hadi nyumbani kwake maeneo ya Kurasini, Dar ambapo alikutwa kwenye maandalizi ya futari ndipo akafunguka.


 Wikienda: Gigy mambo vipi? Tumeamua kukuibukia kwani tuna ubuyu wako sijui kuna ukweli wowote? Gigy: Ukweli gani na ni nani aliyewaelekeza nyumbani kwetu maana ni kitu ambacho sikipendi kabisa waandishi kuja nyumbani na wengi wameshahangaika
kuniomba kuja nyumbani kwetu lakini nimekataa kuwaelekeza. Wikienda: Hili ni gazeti kubwa, hata kama ungekuwa unakaa wapi lingekufuatilia hadi kukupata. Gigy: Mmesema mna ubuyu wangu na mmenikuta kwenye maandalizi ya futari, kuna nini? Wikienda: Kilichotuleta kinaendana na hili suala uliloliongelea, tumepata ubuyu kuwa umepata mwanaume wa Kiarabu anayekupeleka resi kwa kukuwekea masharti juu ya mavazi yako ya kihasara, je, hili likoje? Gigy: Unajua binadamu watakunyima vyote lakini si umbeya, kiukweli nimewakubali sana. Ni kweli kwa sasa nina mtu wangu yupo Dubai lakini sikutaka kumwanika.


 Wikienda: Tunasikia umepewa masharti magumu ya kuvaa nguo za stara ili ubadilishwe dini na ikibidi ufunge ndoa. Gigy: Ukweli kabisa sikutaka kuliweka wazi hili mapema, si unajua wanga wengi lakini wenyewe mnaniona nakaza uzi lakini sijui kama nitaweza kwani mavazi haya (akiwa amevaa baibui) yanahitaji uvumilivu sana ukizingatia mimi mwenyewe mgeni maeneo haya. 

Wikienda: Kwa hiyo umekubali kubadili mavazi? Gigy: Najaribu, nikiweza mtaona kwani naona jamaa ana nia njema na mimi. Wikienda: Ulikutana wapi na mwanaume huyo? Gigy: Ni stori ndefu lakini kwa kifupi alikuwa akiona picha zangu mitandaoni, anazi-like, siku moja akanitumia ujumbe insta direct, tukachati, akaomba namba yangu nikampatia, ndiyo ukawa mwanzo wetu. 

Wikienda: Mna muda gani tangu mmeanza uhusiano? Je, anavyoona habari kwenye magazeti inakuwaje kwa sababu umekuwa ukiripotiwa kutoka na msururu wa wanaume? Gigy: Tuna miezi sita tangu tuanze uhusiano. Kwa nyakati tofauti, Gigy amesharipotiwa kutoka na wanaume wa kada mbalimbali wakiwemo mastaa wa Bongo Fleva, Alikiba, Ommy Dimpoz, Hemedy PHD, Rich Mavoko na wengine kibao

No comments