Header Ads

Gigy Money kumkacha mwarabu wake kwa ubahili

 
VIDEO Queen asiyeishiwa vituko, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amethibitisha kuwa yupo mbioni kumpiga kibuti bwana’ke mwarabu endapo ataendelea kuwa bahili, kwani kwake yeye hakuna mapenzi isipokuwa anachojali ni hela tu. 
 
Akichonga Gigy Money alisema katika maisha yake hapendi mwanaume bahili wala asiye na fedha hivyo kwa kuwa mwarabu huyo ambaye awali alikuwa akimpatia hela nyingi, na sasa anaonekana kumbania kumpa mshiko, atamtosa
muda si mrefu ujao.


 “Siku hizi hakuna mapenzi ya kugandana, mapenzi ni hela, mimi mwenyewe sina hela halafu nikampende mwanaume kapuku tutaendeshaje maisha sasa? Huwa sifanyi biashara hiyo, kikubwa kwangu nampenda mwanaume mwenye mkwanja, mwarabu anazo na mwanzoni alikuwa akinipa za kutosha, lakini sasa naona amekuwa bahili, namuacha,” alisema Gigy Money.

No comments