Header Ads

Hamisa Mobetto aumia jinsi mwanae anavyohusishwa kwenye mambo yasiyomhusu, ‘Issue ya Majay na Lulu’

Mwanamitindo Hamisa Hassani Mobeto, amekataa kuzungumzia mgogoro unaodaiwa kuendelea kati yake na staa wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ huku akionyesha kuchukizwa na jinsi mwanae anavyohusishwa katika mambo yasiyo muhusu.

Hamisa Mobeto akiwa na mtoto wake
Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Mobeto amesema mtoto wake hana hatia yoyote katika mambo yanayoendelea katika mitandao ya kijamii.
“Issue ya Lulu sijui na Majay siwezi zungumzia, kitu ambacho kinaniumiza ni kumwingiza mwanangu kwenye haya mambo, na mtoto wangu anakuwa anajumlishwa katika mambo ambayo hayamuhusu kabisa na hakupaswa kuhusishwa,” alisema Mobeto. Kwa hiyo hakuna mzazi ambae angekubali mwanaye azungumziwe hivyo au aongelewe kwenye mambo yasio mazuri,”
Aliongeza,” Ningekuwa sina mtoto wala nisinge umia lakini kwa sababu kuna mtoto ambaye hana hatia wala hajui kinachoendelea, so sipendi hiki kitu,”
Katika mitandao ya kijamii mashabiki wa Lulu na Hamisa wamekuwa wakitupiana maneno huku chanzo kikidaiwa ni Majay, lakini Hamisa alikataa kuzungumzia chochote kuhusu mpenzi wake huyo wa zamani.

No comments