• Latest News

  June 21, 2016

  HANS POPPE ASEMA YANGA WAMEJITAKIA WENYEWE SUALA LA KESSY


  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesisitiza, lazima Yanga wapate barua kutoka Simba ili beki Hassan Kessy awe huru kucheza Yanga.

  Hans Poppe amesema kipindi cha kuidhinisha usajili kwa Tanzania Bara hakijawadia, hivyo lazima kuwe na barua ya ruhusa kutoka Simba ili Yanga ianze kumtumia katika Kombe la Shirikisho.

  “Yanga wao ni watu wabishi, wanajiona wako juu ya sheria. Hili lingeweza kwisha mapema kabisa, lakini hawakutaka kusikiliza.

  “Tuliwaeleza mapema hilo la Kessy, lakini waliona wanaweza kupita njia ya mkato. Wanasema wao ni timu ya wananchi, ok,” alisema Hans Poppe.

  Yanga iliamua kutowatumia wachezaji wake wake akiwemo Kessy, Andrer Vicent, Juma Mahadhi na Beno Kakolanya kwa kuwa haikuwa na uhakika kuhusiana na suala hilo.

  Hata hivyo kumekuwa na kauli za kuchanganya, awali Caf ilisema ni lazima kupata barua kutoka timu aliyotoka. Kauli ya pili kutoka kwa msemaji wa shirikisho hilo ikaeleza wanaweza kuwatumia lakini lazima iwe makini hasa kama kila kitu kipo kwenye msitari.


  Lakini katika mechi dhidi ya Mo Bejaia, Yanga iliamua kuchukua tahadhari kwa kutomtumia Kessy na wenzake ili kuhakikisha inaondoa hofu hiyo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HANS POPPE ASEMA YANGA WAMEJITAKIA WENYEWE SUALA LA KESSY Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top