Header Ads

Hillary Clinton afikisha wajumbe 2,383 inayohitajika kuwa mgombea urais Marekani
Mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton siku ya Jumatatu (Jana) alifikisha idadi ya wajumbe 2,383 inayohitajika kuwa mgombea wa kike wa kwanza kupata uteuzi wa chama chake cha kuwania nafasi ya urais wa Marekani hii kwa mujibu wa hesabu za wajumbe zilizofanywa na Associated Press.
Ingawa uteuzi wa Clinton hautakuwa rasmi mpaka chama chake kiwe na mkutano mwezi wa Julai.
Mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton ameshinda uteuzi wa chama cha Democrat katika eneo la Puerto Rico.
 

Vyombo vya habari nchini Marekani, vimeripoti kuwa Bi Clinton alishinda kwa asilimia 60% ya kura ikilinganisha na asilimia 35% za mpinzani wake Bernie Sanders
(picha:Getty)

No comments