• Latest News

  June 29, 2016

  Irene Uwoya azua timbwili zito ukumbini na kutolewa nje!

  Ni shida! Staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya hivi karibuni alizua timbwili zito ukumbini lililosababisha atolewe nje na kupelekwa nyumbani kuepusha kuzichapa.
  Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa Irene alizua timbwili hilo hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga jijini Dar ambako kulikuwa na sherehe ya kuagwa (send off) ya mdogo wa msanii mwenzao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’. Mwanadada huyo ambaye alionekana kuwa ‘amekolea kilaji’ alilianzisha mara baada ya kutakiwa kuondoka ukumbini na mhudumu kwani muda ulikuwa umekwisha. 

  “Unajua pale Diamond Jubilee mwisho saa sita, hivyo Uwoya alikuwa amebaki mpaka muda ukapita huku akiwa na wenzake ambapo mhudumu alikuja na kuwaambia wanatakiwa kutoka kwani muda ulikwisha, alipoona Uwoya bado anaendelea kupiga
  ulabu akaenda kumnyang’anya glasi na hapo ndipo timbwili lilipoanzia.


   “Ilibidi marafiki wa Uwoya waingilie kati ili kuepusha shari kwani alikuwa anataka kumshushia kipigo mhudumu huyo ambaye naye alikuwa akimtukana matusi ya nguoni, wakamchukua na kumtoa nje na kuelekea makwao,” kilieleza chanzo. Baada ya kuupata ‘ubuyu’ huo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Uwoya ili kujua ukweli wa habari hiyo ambapo mrembo huyo alikiri kutokea tukio hilo. 

  “Ni kweli tukio hilo lilitokea kwani nilikuwa napata kinywaji lakini ghafla mhudumu alikuja na kuninyang’anya glasi huku akitukana matusi nikapandwa na hasira lakini marafiki zangu waliingilia na kunitoa nje tukarudi nyumbani,” alisema Uwoya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Irene Uwoya azua timbwili zito ukumbini na kutolewa nje! Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top