Header Ads

Audio: Jokate azungumzia dili na Alikiba na Sony na Diamond na tuzo za BET

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, Jokate Mwegelo amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu issue kibao zikiwemo brand yake ya Kidoti na nini kipya kinakuja, muziki wake, mitandao ya kijamii, Alikiba na dili lake la Sony pamoja Diamond na tuzo za BET.


Amezungumza na kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka.
Kuhusu Alikiba na mkataba wake na Sony Music
Watanzania wamsupport tu. Vijana wanapokuwa wanafanya kazi za sanaa na kazi zao zinatambulika kimataifa na wanapata deals za kimataifa ni hatua nzuri kwetu sisi kama nchi na inatia moyo kwa wale wanaochipukia kwamba sanaa inaweza ikawapeleka sehemu mbalimbali duniani na kukutana na watu mbalimbali na wakawa na mafanikio pengine kuliko yale waliyoyafikiria.
Kwahiyo hawa watu tuwachukulie kama watu wanaotufungulia milango, wanatuonesha njia, wanachonga barabara sisi tunafuata tunateleza tu. Sisi ambao tunafuatia inabidi tupige sasa hatua kubwa zaidi ya hapo.
Kuhusu Diamond na BET
Wito wangu wampigie kura Diamond Platnumz aweze kurudisha ushindi nyumbani.
Kwa upande mwingine kuhusu interview hiyo, Jokate aliandika Instagram:
Nimesitisha kufanya interviews kwa muda sasa mpaka nitakapokuwa tayari maswali ni mengi na issues zimekuwa nyingi ❤️❤️❤️ ila hii imebidi tu nifanye kwa heshima sana baada ya kuombwa kwa muda sasa na dada yangu Divine kutoka Njombe na ukizingatia ndio njia ya kwenda kwetu Ruvuma imebidi tu. Ndugu zangu wa Njombe nitasikika live kwenye super mega ya Kings FM leo mchana @kwekadivine @kingsfm radio USENGWILE ❗️❗️❗️#Kidoti.”

Msikilize Jokate hapo chini.

No comments