Header Ads

Kajala hatarini kupata kansa daktari afunguka mazito!STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja, yupo hatarini kupata ugonjwa wa kansa, endapo ataendelea kukiuka masharti aliyopewa na daktari wake juu ya matibabu ya matatizo yake ya ubongo.
Chanzo kilicho karibu na staa huyo, kimetonya kuwa baada ya matatizo yake kugundulika, daktari alimpa dawa ambazo anapaswa kuzinywa saa moja usiku kila siku huku akitakiwa kupumzika kwa muda mwingi, lakini badala yake amebadili muda na pia anapiga ‘ulabu’.

“Kajala asipofuata masharti ya daktari basi siku si nyingi tunaweza kumpoteza au kujikuta akipatwa na maradhi makubwa zaidi. Alikatazwa kunywa pombe, lakini  amemrubuni na kubadilishiwa muda ili apate fursa ya kupiga mitungi.

“Alitakiwa kunywa dawa saa moja usiku, ila ameshindwa, alimuomba daktari ambadilishie muda na kupewa saa 4 asubuhi,” kilisema chanzo hicho.

Inaelezwa kuwa wakati akiomba kubadilishiwa muda, aliomba pia aruhusiwe japo ‘wine’ kidogo, jambo ambalo daktari alimkubalia, lakini kwa sharti la angalau saa tatu kabla hajanywa dawa, abugie maji  lita tatu, kitu ambacho kimekuwa kigumu kwa staa huyo kutokana na kubanwa na ratiba.

Alipotafutwa Kajala mwenyewe ili kuzungumzia hilo, alikiri:
“Ni kweli nilimwambia daktari anibadilishie muda toka usiku na sasa natumia asubuhi, ninajitahidi kufuata masharti na nafuu naiona isipokuwa suala la maji nashindwa maana ninapokunywa ‘gambe’, mpaka muda wa kuniamsha kunywa dawa nakuwa sijanywa maji na daktari aliniambia nisipofanya hivyo naweza kupata kansa,” alisema Kajala.

CHANZO: GPL

No comments