Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge-10

 
ILIPOISHIA: “Tunaomba maji ya kunawa.” Jombi alifutua macho kwa taarifa hizo, akamwangalia mama Mei kwa macho yenye mahaba, wakakutana macho, mama Mei akaachia tabasamu jepesi na kusema... SASA JIACHIE... “NIMEMTUMIA meseji mume wangu...” “Kwamba..?” “Kwamba nakuja hapa baa.” “He! Anakuruhusu?” “Mh! Ananiruhusu lakini lazima kwanza nijipige picha nimtumie kwenye WhatsApp ajue nimevaa vipi wakati nakuja...” “Hapendi uvae vipi?” “Sketi tupu au suruali tupu, hasa usiku. Lakini kwa mchana hapendi nivae kanga, anataka magauni makubwa, unajua umbo langu mimi ni la utata,” alisema mama Mei kwa sauti iliyojaa utulivu... “Oke, sasa ulipokuwa unakuja hapa, mzee Hewa hajakuona?” Mama Mei alikosa raha ghafla, akainamisha kichwa kisha alipokiinua, akasema... “Yule mzee ni kama mbwa.” “Kivipi?”
“Jamani salama hapa?” mzee Hewa alisalimia akivuta kiti na kukaa kwenye meza yao... “Ahaa! Mzee Hewa, karibu sana...sisi tupo salama,” Jombi alichangamka... “Naona uhusiano wenu unakua siku hadi siku,” alisema mzee huyo huku akimwangalia mama Mei kwa macho yaliyojaa msuto na wivu... “Kwa nini mzee Hewa?” swali lilitoka kwa Jombi. Lakini mpaka wakati huo, mama Mei alishajua kuwa, kauli yake ya kusema mzee huyo ni kama mbwa hakuisikia mwenyewe, alimwacha Jombi aendelee kujibu, yeye akainuka kwenda chooni. Baa nzima macho kwake. Maana alipotembea unaweza kusema ataliangusha wowowo au litaanguka lenyewe muda wowote ule. Mzee mmoja yeye alikaa na mkewe, akamkata jicho mama Mei huku akichezesha shingo yake kwa maana ya kufuatilia mdundo wa mwendo... “Baba Nuhu, kwa hiyo wewe uwepo wangu mimi hapa baa huuthamini mpaka unaangalia wanawake vile?” aliuliza mke wa mzee huyo na kumfanya
mumewe kushtuka sana. Wako wanaume walitamani kumfuata mama Mei kulekule chooni ili wajifanye wanaingia kwenye vyoo vya kiume na kumlia taiming nje akitoka waombe namba. Huku baa, wengine walipomaliza kumwangalia mama Mei waliangaliana wao, wateja kwa wateja na kuachia vicheko, wale waliolewa sana bia, waliambiana... “Mzee unacheki zigo, maana’ke lile huna haja ya kudai risiti...” “Acha kabisa! Lazima supu ya pweza ihusike...teh! Teh! Teh!” Kwa upande wake, mzee Hewa pia, licha ya kwamba alishapata japo kwa kubaka, alimsindikiza mama Mei kwenda uani kwa macho yaliyojaa tamaa... “Huyu binti bwana mdogo si wa kukaa pale kwangu, lazima ahame,” alisema mzee huyo... “Kwa nini mzee Hewa..?” “Kesi...huyu binti ni kesi... yaani ukimwangalia tu unajua ni kesi...” “Kesi kivipi mzee Hewa?” “Lazima umbake...wewe unaweza kuishi nyumba moja na binti mzuri kama huyu ukamwacha hivihivi
tu...eti kisa ana mume wake? Ukimwangalia hivi kama amejengwa badala ya kuumbwa. Tena wajenzi wenyewe ni wale mahodari... “Kutoka kifuani kuja kwenye kiuno mwembamba, matiti yake kama hajawahi kunyonyesha na anasema ana mtoto...lakini kutoka kiunoni kwenda chini ndiko kwenye kesi yenyewe. Akitembea yeye juu anakuwa mbele, yeye chini anabaki nyuma... tuache anarudi...mimi naondoka bwana, nilipomuona anakuja huku nikajua yuko peke yake ndiyo maana nikaja, kumbe umeniwahi kijana,” alisema mzee Hewa huku akisimama. Wakati mzee huyo anaondoka, mama Mei anakaa baada ya kusababisha utulivu kwenye baa nzima, mpaka mtu wa kaunta achilia mbali wahudumu wa baa hiyo inayojaza wateja wengi! “Vipi huyu mzee alikuwa anasemaje?” lilikuwa swali la kwanza kwa mama Mei kumuuliza Jombi. Yeye mawazo yake alijua ametoboa siri ya tukio alilosema... “Ha! Hana jipya, anasema alikuona ukija, akajua uko peke yako ndiyo maana alikufuata...”
“Khaaa! Jamani! Huyu mzee ananitafutia nini mimi? Aje anifuate mimi ili iweje kwanza? Yeye ni nani yangu? anikome kabisa,” alisema kwa hasira mama Mei. Mama Mei alikuwa akinywa bia na sasa alikuwa anakunywa ya tatu ambapo lugha pia ilianza kubadilika... “Kawaida huwa unakunywa bia ngapi anti?” Jombi alimuuliza... “Mimi nikinywaga bia tano au sita ndiyo nakuwa vizuri,” alijifagilia, lakini moyoni Jombi alikataa kwa vile alionesha si mzoefu wa bia. “Aisee! Hongera sana anti... lakini mimi leo nataka kutoa dukuduku langu, sijui uko tayari?” Jombi alisema hayo akimwangalia mama Mei usoni... “Kuwa kwangu tayari si inategemea unataka kutoa dukuduku gani anko, mimi niko tayari nakusikiliza...”  Je, Jombi atafungukaje? Nini kitaendelea? Usikose kusoma  Ijumaa ijayo. 

No comments