Header Ads

Kanga Moja Kiunoni...Mbengembenge - 8


ILIPOISHIA : Ni kweli kabisa, wakati Jombi anapita nje ya nyumba hiyo, mama Mei alikuwa akitoka nje kwa lengo la kwenda kwenye baa ambayo Jombi alikuwa anakwenda. Mama Mei yeye alitumwa bia na mume wake... ENDELEA... “ANKO mambo vipi? Upo..?” “Nipo anti, za kwako jamani?” “Mimi mzima, wapi tena mida hii?” “Ah! Nafika hapo kwenye Baa ya Moment nikapoteze mawazo kidogo...” “Aha! Na mimi nakwenda hapohapo, mzee yeye anataka kupotezea mawazo nyumbani,” alisema mama Mei... “Sawasawa, amechoka na kazi...mimi kupotezea mawazo nyumbani siwezagi kabisa,” alisema Jombi huku akimwangalia mama Mei kwa macho ya wazi kabisa kwamba anamzimia ile mbaya. Halafu mama Mei jioni hiyo alivaa t-shirt ndefu kidogo,
ndani alizungushia kanga moja tu, kama kawaida yake, weee! Jombi aliiona nafasi ile ni ya kipekee kujua kama atavuna mahidi au mabua kwa mwanamke huyo, akaanza... “Anti...” “Abee...” “Hivi naweza kupata namba zako za simu ili tuwe tunawasiliana?” Mama Mei alionekana kushangaa kidogo kwa ombi hilo, akauliza... “Anko unataka namba yangu kwa ajili ya mawasiliano gani?” Jombi hakujiandaa na swali kama hilo, lakini akajiongeza na kujibu... “Mawasiliano ya kawaida sana anti, si unajua tena...” “Jamani! Lakini mi sina simu,” alisema mama Mei... “Haiwezekani.” “Kweli tena...mara nyingine huwa natumia simu ya mume wangu ili kuwasiliana na ndugu zangu mbalimbali... labda nikupe hiyohiyo...” “Haa! We nipe hata hiyo, nitafanyaje sasa.” Kweli, mama Mei alimtajia namba za simu ambazo, Jombi alijua ni za mume
wake, baba Mei. Alijua kama angekataa angempa maswali mengi mwanamke huyo wakati yeye alisema ni namba ya mawasiliano tu. Jombi alizisevu namba hizo, akaandika ‘Kanga Moja Mbengembenge.’ Wakati wanakaribia kuingia kwenye baa, mama Mei akasema: “Utume meseji basi ili niione namba yako.” Jombi alishangaa... “Huyu si amesema anatumia simu ya mume wake, sasa nitume meseji kivipi?” alijiuliza, lakini akasema moyoni atatuma tu, kama atakamatwa si yeye mwenyewe bwana! “Oke, natuma, yangu inaishia na hamsini na tano,” alisema Jombi... “Oke...nitakucheki basi,” mama Mei alihitimisha kusema huku wakiachana, mama Mei alikwenda kaunta, Jombi alikwenda kukaa kwenye kiti. Jombi akiwa anapata moja moto, moja baridi, alifikiria sana kuhusu kumtumia meseji mama Mei lakini moyoni mwake alikiri kuwa, mwanamke huyo ametokea kumpenda kuliko hata mke
wake. Alikuwa tayari ndoa ya mama Mei ivunjike na yeye pia ivunjike, yeye na mama Mei waishi pamoja. Mwishowe, Jombi aliamua kumtumia meseji mama Mei... “Namba yangu ni hiyoJombi hapa.” Mama Mei alikuwa akipika msosi wa usiku, mume wake alikuwa sebuleni akiendelea na zile bia zake. Mama Mei alishika simu haraka ili kusoma meseji iliyoingia... “Namba yangu ni hiyo-Jombi hapa,” mama Mei aliisoma meseji ya Jombi akaachia tabasamu laini huku akiwa makini na mazingira ya pale ili isijekuwa mumewe akatokea ghafla na kumnasa akisoma meseji za wanaume. Akamjibu Jombi... “Poa, mimi napika.” “Mh! Nije kula mama?” Jombi alirudisha majibu. Mama Mei aliachia tabasamu tena, hasa baada ya kusoma lile neno ‘mama’ alilolitumia Jombi kumwita... “Huogopi?” aliuliza mama Mei... “Kimtindo.”
“Mtindo gani?” “Yaani kiaina, naweza kuja kula kama utanikaribisha wewe mwenyewe.” “Mh! Unamjua unamsikia..?” “Nani?” “Mume wangu...” “Nakuja kama kaka yako...” “Mbona kwenye harusi hukuja?” “Teh! Teh!” alicheka kwa sauti Jombi lakini akatuma meseji hiyohiyo ya kicheko. Mama Mei naye alichekea moyoni, akamjibu... “Umeona ee? Labda nikupakulie chakula chako kwenye hotpot kama hutajali,” alisema mama Mei. Jombi alijua utani, lakini akajibu haraka sana... “Niko tayari kama ni kweli.” Kuanzia hapo, mama Mei hakujibu tena meseji za Jombi na ukimya huo ulitawala kwa muda huku Jombi akiendelea kutumatuma meseji za hapa na pale zenye mlengo wa uchokozi. Je, kiliendelea nini? Usikose kusoma siku ya Ijumaa,


Mtunzi
Irene Mwamfupe Ndauka

No comments