Header Ads

KESHO TFF KUIKUBALIA YANGA IFANYE UCHAGUZI WAKE, ITATOA VISINGIZO HIVI..


RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatarajia kukutana na seretarieti ya Yanga, kesho.

Taarifa zinaeleza, TFF haitakuwa na ujanja zaidi ya kuiruhusu Yanga ifanye uchaguzi wake tofauti na ilivyokuwa ikishikilia msimamo wake kupitia kamati ya uchaguzi.

Yanga imekuwa ikiomaa kutaka kufanya uchaguzi wake kwa kuwa ni kwa mujibu wa katiba ya Yanga.

Lakini TFF imekuwa ikisisitiza ina haki ya kufanya hivyo, jambo ambalo linaonekana kukosa mashiko.

Tayari Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ametangaza Rais wa TFF, Jamal Malinzi atazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na suala hilo.

Lakini habari za uhakika zinaeleza Malinzi, atatangaza kuwapa nafasi Yanga kufanya uchaguzi wao kwa kufuata utaratibu ambao ni sahihi.

TFF itatoa mikono yake na kuipa Yanga imalize jambo hilo na huenda suala la “Yanga iko katika michuano ya kimataifa”, ndiyo litakuwa neno la TFF kutaka kuipa Yanga nafasi iendelee na uchaguzi wake.

Wakati uamuzi huo wa TFF unaibuka, bado kuna tuhuma nzito kwa shirikisho hilo kwamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya TFF, Alloyce Komba na viongozi wa BMT wanatuhumiwa kutaka kumng’oa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na msaidizi wake Clement Sanga.


Tayari Yanga imewasilisha malalamiko yake kuhusiana na suala hilo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Kati ya viambatanisho ni mkanda ambao una sauti zinazoelezwa kuwa ni za wahusika wakipanga namna ya kumg’oa Manji kwa figisu. 

No comments