• Latest News

  June 09, 2016

  Kifaa cha kudhibiti matumizi ya fedha chazinduliwa  Kampuni mmoja ya uingereza inatarajia kuweka kifaa kinachodhibiti matumizi ya pesa kwa kuwapatia wateja wake mshtuko wa umeme iwapo watapitisha kiwango cha matumizi yao.

  Kampuni ya Intelligent Environments,imezindua mfumo ambao utaiunganisha na mpiro wa kuvaliwa mkononi wa Pavlok ambao unatoa mshtuko wa volti 255 kwa akaunti ya benki,iwapo fedha katika akaunti zitashuka kupita kiwango mteja alichokubali.
  Pia mpira huo una uwezo wa kufanyakazi na mita za umeme kuzia matumizi ya juu ya umeme na kuokoa bili iwapo fedha hizo zitashuka.

  Mtendaji mkuu wa kampuni Intelligent Environments,David Webber ameiambia BBC Wazo hilo lilikuwa kuhusu mapendekezo ya wateja.

  Hakuna benki yoyote imetangaza itaazisha mfumo huo kwa wateja wake lakini benki hiyo ya mtandao ya Intelligent Environments imetaja benki kadhaa za uingereza kama wateja wao ambao wanatumia mifumo yake ya mitandao.
  Image copyright AFP
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Kifaa cha kudhibiti matumizi ya fedha chazinduliwa Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top