Header Ads

Lulu Diva: Nikiporwa mpenzi wangu, nalipiza bila kujali lolote!

VIDEO Queen asiyeishiwa na vituko Bongo, Lulu Diva amefunguka kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya mastaa kupora mabwana wa wenzao ila kwa atakayemfanyia mchezo huo atalipiza bila kujali lolote.

 
Lulu alifunguka hayo baada ya kutuhumiwa kunyakua mpenzi wa dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Grace ambapo inadaiwa kajimilikisha mwanaume huyo wakati akijua ndiye anayemuweka mjini shosti wake huyo.
“Yaani Lulu hana hata aibu, kuna dada mmoja ni rafiki yake, anaitwa Grace. Yule dada alikuwa na jamaa yake anayemuweka mjini, cha ajabu Lulu sijui wamekutana wapi na mwanaume huyo, kamchukua na sasa yuko naye,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kupata ubuyu huo, mwandishi wetu alimtafuta Lulu alipopatikana alisema kwa shari: “Kinamuuma ee, yeye aliponichukulia wangu alidhani nimefurahi? Sasa kwa taarifa tu ni kwamba mimi anayenipora bwana wangu, siku wake akinikalia vizuri nalipiza.”

CHANZO; GPL

No comments