Header Ads

Mama, Baba Wamtenga Wolper kisa Skendo za Wanaume… Jacqueline Wolper

DAR ES SALAAM: Jacqueline Wolper, staa wa Bongo Muvi, ametengwa na familia yake akiwemo mama na baba yake mzazi kutokana na kukabiliwa na skendo za wanaume kila kukicha.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, staa huyo alisema migogoro yote ambayo inatokea kwenye familia yake ilianza mara tu baada ya kuachana na mchumba wake ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayejulikana kwa jina moja la Putin.
Harmonizer-na-Wolper 
Jacqueline Wolper na Harmonizer.
Alisema mwanaume huyo ndiye anayezungumza uongo kwenye familia yake na kumsababishia aonekane ni mbaya kwa ndugu zake hadi kufikia hatua ya kumtenga.
“Unajua nilipoamua kushtuka na kuachana na Mkongo kumekuwa kunaibuka vitu vingi sana katika familia yangu kwa sababu yeye anajifanya ni mwema kwao na kila anachozungumza wanaona kuwa anasema kitu sahihi lakini kumbe ni mzushi tu, amewajaza maneno kibao kuhusu mimi na wanaume,” alisema Wolper.
Staa huyo alizidi kufunguka kuwa, baada ya kuamua kuachana na Mkongo huyo kwa kitendo alichomfanyia hasa cha kumtelekeza hotelini Afrika Kusini, ameamua kutulia na mpenzi wake wa sasa ambaye pia ‘anachafuliwa’ na Mkongo.
wolper-4Jacqueline Wolper na Mkongo.
“Najua kabisa kinachomuuma Mkongo ni mimi kuwa na mpenzi mwingine lakini nashangaa sana maana yeye alinitumia ndivyo sivyo sasa matokeo yake nilipochoka na kuamua kuendelea na vitu vyangu ndiyo anawaambia vitu vya uongo mama yangu na ndugu zangu, wanatengeneza sumu ya kunichukia mimi,” alisema Wolper.
Akizidi kutema cheche kwenye kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, Wolper alisema alimsihi mpenzi wake huyo wa zamani (Mkongo) kumuacha na familia yake kwa sababu mapenzi yalishaisha zamani, asimharibie nyumbani kwao na akumbuke wale ni ndugu zake wa damu, ipo siku watakaa na kuyamaliza.
“Namshangaa sana kwa kweli, akumbuke kabisa jitihada anazofanya kuniangusha na hata kuniaibisha zitagonga mwamba tu kwa kuwa sumu anayoieneza kwenye familia yangu mwisho itakuwa aibu yake kwa kuwa wale ni damu zangu, nitayamaliza yeye atabaki na aibu,” alisema Wolper.
Kabla ya kuachana na Mkongo na kuhamishia majeshi kwa mpenzi wake wa sasa, Wolper alishawahi kutembea na mfanyabiashara maarufu kwa jina la Dallas ambaye alimwagana naye baada kushindwana tabia licha ya kuwa alishambadilisha hadi dini Wolper na kuwa Muislam.

No comments