Header Ads

Mfumo wa Kidigitali wa Kusoma Magazeti ‘M-Paper’ Wazinduliwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa Uzinduzi wa Mfumo mpya  wa kidigitali wa M-Paper kwa kushirikiana na Smart Codes unaowezesha wateja wa mtandao huo wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta, kuweza kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu  bei ya nakala halisi ya gazeti au jarida, Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa kampuni hiyo, Saurabh Jaiswal na Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno.
????????????????????????????????????Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Saurabh Jaiswal(kushoto)na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mfumo mpya wa kidigitali wa M-Paper unaotolewa na Vodacom Tanzania kwa ushirikiano wa Smart Codes unaowezesha wateja wa mtandao huo wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta, kuweza kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu bei ya nakala halisi ya gazeti au jarida.
????????????????????????????????????Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno(katikati)akiwaelezea waandishi wa habari jinsi ya kupakua bure program ya M-Paper kwenye simu, Wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo mpya wa kidigitali unaotolewa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Smart Codes unaowezesha wateja wa mtandao huo wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta, kuweza kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu bei ya nakala halisi ya gazeti au jarida.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa Vodacom Tanzania, Saurabh Jaiswal na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia.
????????????????????????????????????Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno (kushoto) akiwaelezea waandishi wa habari jinsi ya kupakua bure program ya M-Paper kwenye simu, Wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo mpya wa kidigitali unaotolewa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Smart Codes unaowezesha wateja wa mtandao huo wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta,kuweza kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu bei ya nakala halisi ya gazeti au jarida.Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia.
????????????????????????????????????Baadhi ya wawakilishi wa vyomba mbalimbali vya habari vya  magazeti wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (wasabi kushoto) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno(wasita kushoto)wakati wa Uzinduzi wa Mfumo mpya  wa kidigitali wa M-Paper unaotolewa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Smart Codes unaowezesha wateja wa mtandao huo wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta, kuweza kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu  bei ya nakala halisi ya gazeti au jarida.
Unaowezesha kupata habari za magazeti kupitia simu za Smartphone na kompyuta
Dar es Salaam, Tuesday, June 21, 2016. Katika kutimiza dhamira yake ya kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia leo kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua mfumo mpya  wa kidigitali wa M-Paper unaowezesha wateja wanaotumia simu za Smartphone, na kompyuta kuweza kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu  bei ya nakala halisi ya gazeti au jarida.
Kwa kutumia mfumo huu wa M-Paper. Vodacom imelenga kuwawezesha wateja wake kupata taarifa zinazoandikwa kwenye magazeti na majarida wayapendao kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi. Programu inaotumika katika mfumo huu ambayo imefanikishwa kwa ushirikiano wa kampuni ya kidigitali ya Smart Codes na Vodacom  inapatikana kwa kupakuliwa (download) bure katika tovuti ya http://mpaper.vodacom.co.tz/
Pamoja na wateja kuweza kupakua bure programu hii, watakapokuwa wanahitaji kusoma magazeti watalazimika kulipia nusu  ya bei ya gharama ya nakala halisi kwa gazeti atakalohitaji kusoma mteja, baada ya kupakua programu na kuchagua gazeti alipendalo kuna maelekezo ya kulipia kabla ya kuanza kusoma ambapo gharama za usomaji zinakatwa kwenye fedha ya muda wake wa maongezi au kulipia kwa njia ya M-Pesa ambapo wasomaji waliopo nje ya nchi wanaweza kulipia huduma hii kupitia kadi za kimataifa za kufanyia mihamala ya malipo (Debit Card/Credit card)
“Vodacom Tanzania kwa mara nyingine tumedhihirisha dhamira yetu ya kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa  kuanzisha huduma hii mpya ya aina yake ya kuwawezesha watanzania kupata taarifa kupitia simu zao. Huduma hii pia ni mwendelezo katika kurahisisha maisha kwa wananchi ikiwemo kubadilisha maisha ya watu kwa kupanua wigo wa ajira nchini kama ambavyo  wabunifu wa programu hii wameweza kuitumia  kurahisisha maisha.”.Alisema Rosalynn Mworia,Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania.
Mworia alisema tayari magazeti na majarida zaidi ya 52 yanapatikana katika programu hii ambao wateja wanaweza kuanza kujisomea kwa gharama nafuu ya nusu bei ya nakala halisi ambapo pia wanaweza kuchagua namna ya kulipia kupata huduma hii ambapo mteja anaweza kulipia kwa wiki,kwa mwezi au kwa mwezi.
Kwa upande Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno alisema kuwa wameamua kushirikiana na Vodacom kuleta huduma hii ya aina yake inaowezesha watanzania kupata taarifa kwa urahisi na kwa gharama nafuu baada ya kuona mtandao wa Vodacom umejipanga kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora kwa kutumia ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia kupitia simu za mkononi.
“Hivi sasa tunaishi katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia na teknolojia imekuwa ikibadilika siku hadi siku ambapo hivi sasa mifumo mingi inayotumika ni ya kidigitali,hivyo ushirikiano wetu na Vodacom katika kuanzisha programu hii ya M-Paper na kuhakikisha inawafikia wateja wote wanaotumia simu za SmartPhone ni ubunifu wa aina yake katika kuhakikisha taarifa na habari zinawafikia wanajamii kwa njia rahisi na ya haraka  na kwa gharama nafuu.

No comments