Header Ads

Monalisa akanusha kuwa mjamzitoLICHA ya tetesi kuzagaa kama ‘kimbunga’ kuwa mkongwe wa filamu Nollywood, Monalisa Chinda (40) mjamzito, staa huyo ameibuka na kukanusha madai hayo.
Monalisa ambaye Februari mwaka huu alifunga ndoa ya kimila na Victor Tonye Coker alisema kuwa ndoa ni kitu kizuri na anafurahi kuwepo hivyo lakini kuwa mjamzito si kweli kwa sasa.
“Ndoa ni nzuri namshukuru Mungu. Lakini habari kuwa mimi ni mjamzito inayoendelea kusambaa si kweli. Inawezekana nikawa na mtoto hivi karibuni lakini ni Mungu ndiye anapanga itokee,” alisema Monalisa aliyewahi kubamba na Filamu ya The Unthinkable.

No comments