• Latest News

  June 30, 2016

  Msanii aliyetekwa Nigeria apatikana


  Polisi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wamempata msanii maarufu ,Ado Daukaka,aliyepotea siku ya Ijumaa.
  Wanasema wamemkuta akiwa katika hali ya kutokuwa na fahamu huku akiwa amekonda sana.
  Daukaka ameiambia BBC kuwa alitekwa nyara na kundi la watu waliokuwa na hasira kutokana na wimbo aliouandika uliokuwa unawazungumzia viongozi wa siasa wanajihusisha na rushwa.
  Amesema walimuweka ndani kwa siku mbili bila ya kumpatia chakula na kisha kumtelekeza msituni.
  Kwa sasa anaendelea na matibabu katika hospitali moja iliyopo kilomita 120 kutoka eneo alilotekwa.
  Mojawapo ya nyimbo zake ni unaoitwa kwa lugha ya Kihausa Gyara kayanka, ukimaanisha ''tunapaswa kufanya matendo mema'' unaowazungumzia wanasiasa wanaotoa ahadi nzuri bila kuzitimiza.

  CHANZO; GPL
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Msanii aliyetekwa Nigeria apatikana Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top