Header Ads

Pam D aahidiwa darasa la Hip Hop na R.O.M.A


MKALI wa Miondoko ya Hip Hop, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A’ amefunguka atampa darasa la Hip Hop, staa wa Bongo Fleva, Pam D ili aweze kuchana mistari kama afanyavyo yeye.
romaIbrahim Musa ‘R.O.M.A’
Akipiga stori na safu hii, R.O.M.A alisema mdada huyo amekuwa akitaka awe mchanaji mzuri hivyo ameamua kumfundisha ili wawe wanakamua pamoja kwenye shoo mbalimbali kwani anahisi ana damu ya Hip Hop.
“Niko karibu sana na Pam, nimepanga kumfundisha kuchana ili awe kama mimi kwani najua anaweza. Kwa mfano Julai 7, mwaka huu tutapanda jukwaa moja kule Ngonga Beach Resort pande za Mbeya pamoja na akina Mesen, Kadja Nito na Msami  Baby. Kolabo yangu na yeye itanogaje siku hiyo!” alisema R.O.M.A ambaye siku za hivi karibuni amekuwa ‘klozi’ na mwanadada huyo.

No comments