Header Ads

Penina amwaga chozi kisa kudaiwa kujiingizaJennifer Raymond ‘Penina’

MSANII wa Bongo Muvi anayefanya poa, Jennifer Raymond ‘Penina’ hivi karibuni alijikuta akitokwa na machozi baada ya kudaiwa kujiingiza katika biashara ya kujiuza nchini China.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Penina amekuwa na safari za China na Thailand na kwamba mambo yake kwa sasa ni supa.
penina“Yaani safari kwake haziishi, kama siyo China basi Thailand na inasemekana kuwa huko huwa anakwenda kujiuza na kupata fedha,” kilisema chanzo.
Baada ya madai hayo, Amani lilimtafuta Penina na alipopatikana alifunguka;
“Jamani! Jamani! Mimi sijui hata wanajiuzaje? Huwa nakwenda kule kibiashara tu. Ndiyo matatizo ya Wabongo, mwanamke akijishughlisha na kupata mafanikio wanasema anajiuza,” alisema Penina huku akilia.

CHANZO: GPL

No comments