• Latest News

  June 14, 2016

  Polisi Wamhoji Zitto Kabwe Kwa Dakika 90

  Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe  asubuhi ya leo June 13 2016 alikutana na wanahabari na kuzungumzia kuhusu polisi kuzuia kongamano ambalo liliandaliwa na chama hicho ili kujadili bajeti. Pia alizungumzia kuhusu yeye kusakwa na polisi kwa kuviziwa na sio kwa utaratibu wa wito.

  Jana jioni  Zitto Kabwe alipokea wito wa kuhitajika Central polisi kwa mahojiano ambayo yalichukua zaidi ya dakika 90 .
  Baada ya  kutoka kwenye mahojiano aliyepata nafasi ya kuzungumza ni wakili wa chama hicho Steven Mwakibolwa ambaye ameeleza sababu za wito huo kituoni hapo.

  "Wamechukua maelezo ya Zitto kufuatana na kongamano la chama lililokuwa limezuiliwa jana.Baada ya mahojiano na mazungumzo na polisi, chama kitatoa taarifa rasmi juu ya nini kitafuta baada ya hapa." Amesema Mwakibolwa

  "Kama alivyoeleza mwanasheria tumemaliza mahojiano na polisi kwa hiyo kesho tutatoa kauli yetu ya hatua inayofuata, nimeitwa polisi nimekuja, wanachama watulie tunaendelea na majadiliano na polisi ili tuendelee na kazi zetu za kisiasa kama kawaida" Amesema Zitto Kabwe
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Polisi Wamhoji Zitto Kabwe Kwa Dakika 90 Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top