Header Ads

Polisi Wavamia Nyumba ya Faiza Ally na Kupekuwa Kila Kona baada ya Kupata Taarifa Anajiusisha na Madawa ya Kulevya

Mrembo na muigizaji machachari Faiza Ally, amedai kuwa mapema siku ya leo alifatwa na askari Polisi zaidi ya Saba nyumbani kwake wakimtuhumu kuwa anafanya biashara haramu ya ‘Madawa ya kulevya’. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza amesema Polisi hao walifanya upekuzi na hawakupata chochote cha zaidi.

Leo tarehe 3/June/2016 Kwa Kweli ni siku ambayo sitakuja kuisahau kwenye maisha yangu-wamekuja maaskari saba kwangu wakiwa na silaha!!! Eti wamepata taarifa eti mimi nabeba madawa ya kulevya kweli? MANGE kila siku anawataja wahusika lkn sijui Kama wanafatiliwa leo nafatiliwa mtu kama mimi ambaye sijawahi wala kuwaza nifanye hivyo? Kweli mtu unatoka kwako kwenda kutoa taarifa za uongo bila kuwa na uhakika wala uthibitisho wowote! Kwa Kweli nimewanyanyulia mikono walimwengu ila nimesikitishwa sana Kwa yoyote alienda kupeleka taarifa hizo police amekosea sana Na InshaAllah M.Mungu atamuathibu Kwa namna ambayo anaijua yeye! Mimi sijui walimwengu mnanionaje ? Natamani mnijue nikoje! LIFE IS NOT FAIR……lkn Kama muonekano wangu Ndio unanifanya nishukiwe kuwa najihusisha na madawa! Kama ni muonekano wangu unanifanya nionekana malaya! Kama ni muonekano wangu unanifanya nikashifiwe Basi wallah sitabadilika Kwa kuwa naamini M.Mungu ameniumba hivi Kwa sababu ntaendelea kuwa mimi siku zote na sintabadilika kamwe Maana MUNGU HAJAWAHI KUNIANGUSHA HATA SIKU MOJA NA HATA NIANGUSHA KAMWE……… Poleni sana mliopeleka taarifa za uongo police nimesachiwa kwangu bila hofu yoyote huku nikiwa nimekabithi maisha yangu mikononi Kwa M.Mungu Japo nilikua na hofu ya kuwa huenda kuna mtu amenichukia labda anataka kunipa kesi lkn mwisho wa siku nimekua mshindi Kwa mara nyingine na si kwamba nina uwezo ila ni Mungu tu na usafi wa moyo wangu ! NARUDIA TENA NATAMANI WATANZANIA NA ULIMWENGU WANIJUE NIKOJE – LKN NAKUBALI TENA KWA MARA NYINGINE LIFE IS NOT FAIR… #Regrann

No comments