• Latest News

  June 06, 2016

  Sakata la Manji, Mwenyekiti TFF afikishwa Takukuru


  BARAZA la Wazee la Yanga, limeamua kupeleka sauti za Mwenyekiti wa Uchaguzi  wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwenye makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

  Sauti hizo ni zile ambazo Alloyce Komba anatuhumiwa kwamba alikuwa akipanga mbinu za kumhujumu Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.
  Taarifa za uhakika kutoka Yanga zinaeleza, wazee hao wakiongoza na katibu wao, Yahaya Akilimali watatua Takukuru leo kufanya kazi hiyo ili sheria ichukue mkondo wake.
   “Nimeambiwa na wazee wenzangu kwamba Jumatatu tunakwenda kufanya kazi hiyo ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake,” alisema mmoja wa wazee wa Yanga alipozungumza na Championi Jumatatu.
  Tayari Komba ametangaza kukaa pembeni ili uchunguzi kupitia tuhuma hizo uchukue mkondo wake.
  Uongozi wa Yanga uliahidi suala hilo litafikishwa kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Sakata la Manji, Mwenyekiti TFF afikishwa Takukuru Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top