Header Ads

Serengeti Boys inahitaji sapoti kubwa


 
TIMU ya Serengeti Boys juzi ilifanikiwa kubuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Shelisheli kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michezo ya Afrika.
 
 Haya ni matokeo mazuri kwa timu hiyo ambayo kwa siku za hivi karibuni
imekuwa ikionyesha kiwango kizuri. Timu hii sasa itatakiwa kwenda kucheza mchezo wa marudio na ikifuzu itapambana na timu ya taifa ya Afrika Kusini. 
 
Championi tunaamini kuwa timu hii inaweza kufanya vizuri zaidi ya hapo kama itaungwa mkono kwa nguvu kubwa na serikali pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). 
 
Kwa kuwa kwa sasa hakuna timu nyingine ya taifa ambayo inaonyesha mwanga wa mafanikio ilikuwa vyema kama nguvu yote ingehamishiwa huku ili tuweze kuwa na kitu cha kujivunia. Msingi wa soka letu ni vijana na hivyo itakuwa vizuri kama nguvu kubwa itawekwa huku ili hawa wakawe faida kwetu kwa siku za usoni.

No comments