Header Ads

Serikali na upinzani Kenya zaandaa sherehe tofauti sikukuu ya Madaraka leo

Hii leo Kenya inaadhimisha sikukuu ya Madaraka.
Serikali imeandaa sherehe maalum za kitaifa katika mji wa Nakuru ulioko katika bonde la ufa takriban kilomita mia mbili kutoka mji mkuu Nairobi.
Hii ndio mara ya kwanza kwa sherehe hizo kuandaliuwa nje ya mji mkuu wa Nairobi.
Rais Uhuru kenyatta na naibu wake William Ruto tayari wamewasili huko Nakuru na kukagua guaride la heshima.

Image captionRais Uhuru kenyatta na naibu wake William Ruto tayari wamewasili huko Nakuru na kukagua guaride la heshima.

Hata hivyo kutokana na joto la kisiasa lililopanda katika siku za hivi majuzi, muungano wa upinzani unaongozwa na Raila Odinga nao umeandaa sherehe mbadala katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi kuonesha tofauti zao na serikali inayoongozwa na rais Uhuru Kenyatta.
Muungano huo ulipata afueni hapo jana baada ya mahakama nchini Kenya kutoa uamuzi kwamba muungano huo wa upinzani CORD una haki ya kuandaa mkutano wa hadhara kusherehekea siku hiyo pia kulingana na katiba ya taifa.
Upinzani ulikuwa umewasilisha kesi mahakamani baada ya serikali kupiga marufuku mkutano huo wa hadhara kwa sababu za usalama.

Image captionWafuasi wa upinzani wakiwa katika bustani ya Uhuru Nairobi

Hata hivyo jana jioni viongozi wa upinzani walifanya mkutano wa hadhara na rais Kenyatta katika ikulu ya Nairobi na kutangaza kuwa walikuwa wamekubaliana mbinu za kutanzua mzozo kuhusiana na uhuru wa makamishna wa tume huru ya uchaguzi ya Kenya IEBC.
Jijini Nairobi mwandishi wetu David Wafula aliyeko katika bustani ya Uhuru, wafuasi wa muungano wa upinzani CORD wameanza kuwasili wakisuburi viongozi wao kuwasili katika mkutano huo wa hadhara.
Hali ya usalama imeimarishwa.

Image captionMfuasi wa upinzani katika bustani ya Uhuru Nairobi

Maafisa wa polisi, wamekuwa wakipekua kila mtu ambaye anaingia katika bustani ya Uhuru.
Hata hivyo kuna ripoti kwamba watu watano wameshikwa na polisi wakijaribu kuingia katika mkutano huo na silaha hatari zisizokubaliwa.
Silaha hizo zinaaminika kujumuisha rungu na panga
CHANZO: BBC SWAHILI

No comments