Header Ads

UJERUMANI YAANZA EURO KWA KUTOA KIPIGO CHA MABAO 2-0 KWA UKRAINE


Kiungo mkongwe wa Manchester United, Bastan Schweinsteiger ameingia katika dakika 10 za mwisho za mchezo na kuihakikisha timu yake ya taifa ya Ujerumani ushindi wa kwanza wa michuano ya Euro 2016.

Ujerumani imeifunga Ukraine kwa mabao 2-0 ikiwa ni mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo.

Ilikuwa mechi ngumu, pamoja na kuongoza muda mrefu, lakini Ukraine walionekana ni hatari na kama wangesawazisha wakati wowote.

Lakini bao hilo la dakika za mwisho kabisa la Schweinsteiger likamaliza kabisa ubishi na kuwamaliza kabisa wachezaji wa Ukraine walioonekana kupambana bila ya kuchoka hata kidogo tokea mwanzo.


No comments