• Latest News

  June 14, 2016

  UJIO WA NYOTA HUYU YANGA WAMWEKA ROHO JUU TAMBWE

  Mshambuliaji wa Yanga Amiss Tambwe amesema hana hofu ya kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga kufuatia ujio wa wachezaji wapya Yanga.

  Walter Musona

  Yanga inakaribia kuinasa saini ya mshambuliaji hatari kutoka nchini Zimbabwe, Walter Musona ambaye anamudu kucheza nafasi ya Tambwe.

  Kwa upande wake Tambwe amesema hana hofu yoyote ya kupoteza namba katika kikosi cha kwanza Yanga lakini akikiri kuwa soka ni mchezo wa ushindani hivyo kujituma kwake ndo kutamhakikishia nafasi klabu hapo.

  Tambwe
  "Soka ni mchezo wa ushindani kwa timu na timu, wachezaji kwa wachezaji, kama mchezaji siku zote nipo kwa ajili ya kuisaidia timu yangu, lakini pia ushindani kutetea nafasi yangu uwanjani" alisema Tambwe.

  "Nawakaribisha wachezaji wapya kwa ajili ya kuipigania Yanga, lakini hitakuwa rahisi kupoteza nafasi yangu." aliongeza.

  Tambwe alijiunga na Yanga akitokea Simba na amekuwa na uzoefu mkubwa katika ligi kuu Vodacom huku akifanikiwa kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa ligi hiyo msimu huu kwa kufikisha jumla ya magoli 21 katika ligi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UJIO WA NYOTA HUYU YANGA WAMWEKA ROHO JUU TAMBWE Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top